WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WALAANI WANAURUSHA PICHA CHAFU MTANDAONI
Mkurugenzi Mtendaaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu Nchini Tanzania LHRC Bi Hellen Kijo Bisimba akizungumza na wanahabari mapema leo |
Mashirika
yanayofanya kazi ya utetezi wa haki za binadam hasa zinahusu makundi maalum ya
watoto na wanawake wamejitokeza na kulaani vikali vitendo vya kuchapisha picha
na video chafu katika mitandao ya kijamii.
Akizungumza
na Waandishi wa habari mapema hii leo kwa niaba ya watetezi hao, Mkurugenzi wa
kituo cha sharia na haki za Binadamu Bi Kijo Bisimba amesema hivi sasa watu wamekuwa
wakitumia mitandao ya facebook,instagram,blog na whatsapp kutupia picha
mbalimbali zinazokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania
Amesema
picha nyingi zinazorushwa katika mitandao zimekosa maadili, utu,na zimekuwa
zinaingilia faragha za watu jambo ambalo linakwenda kinyume na katiba ya
Jamuhuri ya muungano wa Tanzania sambamba na kukiuka haki za binadamu.
Ametaja
baadhi ya matukio ambayo yamesambazwa katika mitandao ya kijamii lakini
yamekiuka maadili ni pamoja vifo vya mama na motto kilichotokea Bagamoyo mnamo
tarehe Mei 4,2016 ambapo picha zilipigwa na kuonyesha miili ya marehemu ikiwa
na majeraha ya kutisha kwa kitendo walichofanyiwa.
Tukio lingine
ni lile lilitokea Mkoani Kilimanjaro ambapo mtoto alipigwa picha na kuzituma
katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwa katika jeneza baada ya kuuwawa
na mama yake wa kambo.
Mbali na
tukio hilo pia, DKT Bisimba amesema wamesikitisha na tukio la kumuonyesha utupu
wa mtu mmoja aliyedaiwa kuwa Msukule baada ya kukutwa katika kisima kimoja huko
Kibamba jijini Daresalaam na kusema si
maadili kuonyesha utupu wake.
“Chukulia
kuwa yule ni mama yako Dada yako amekutwa hivyo na kupigwa picha za utupu
ungejisiakije, lazima watu wabadilike na serikali ichukue hatua katika masuala
haya”Alisema Bisimba.
Katika
hatua nyingine, Bi Bisimba ameitaka jamii kuacha kabisa tabia ya kuwavunjia
makundi ya watoto na wanawake kwani picha zinazorushwa katika mitandao
zinawaathiri wahusika na kuchochea maumivu ya kihisia kwake na ndugu wa familia
yake.
Aidha
kwa upande wa Serikali, watetezi hao wa haki za binadamu wameitaka serikali
ichukue hatua kali za kisheria kwa wanaotumia mitandao vibaya bila ya kujali
vyeo vyao.
Wanahabari wakiwa kazini |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni