WAFANYABIASHARA WA KARIKAOO MWISHO MEI 8,NI WALE WANAOFANYA BIASHARA BARABARANI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Wafanyabiashara wa Kaliakoo ambao wanatakiwa kuondoka Kabla ya Mei 8 mwaka huu |
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imewataka
wafanyabiashara wote wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi wawe
wameondoka kwenye maeneo hayo kabla ya mei 8 mwaka huu,lasivyo halmashauri hiyo
itawachua hatua za kinguvu kuwaondoa katika maeneo hayo.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Akitangaza uamuzi huo,mbele ya Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, saya Mnguruni amesema wanafanyabiashara wanatakiwa kuodoka kwenye maeneo hayo kutokana na halmashauri hiyo kutenga maeneo maalum yenye huduma stahiki kwa wafanyabiashara hao zaidi ya 2961,
Mnguruni ameyataja maeneo hayo yaliyotengwa ni pamoja na Tabata Muslim, Ukonga, Kivule, na Kigogo Fresh.
Mkurugezi huyo
amebainisha kuwa maeneo hayo
yaliyotengwa yanauwezo wa kuchukua wafanyabiashara zaidi ya 6000 na yana huduma
zote stahiki huku akiongeza kuwa maeneo hayo yatawekewa vituo vya daladala ili
yaweze kufikika kiurahisi.
No comments
Post a Comment