HATIMAYE TSN HYPERMARKET YAWASOGEZEA FURAHA WAKAZI WA MWANZA,SOMA HAPO KUJUA
Turn off for: Swahili
Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage akikata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa TSN Hypermarket Rock City Mall, Mwanza.
|
WAKAZI
wa Mwanza wajidai, TSN imefungua Hypermarket mbayo ni tawi jingine
jipya la TSN mjini Mwanza, Hypermarket hii inayoendelea kutoa huduma kwa
wakazi wa Mwanza imefunguliwa kuwafikia wakazi wa Mwanza waliokuwa
wakikosa uhondo wa bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu zikiwemo mbogamboga
fresh kutoka hapa hapa nyumbani.
Akizungumza
katika ufunguzi huo Mkurugenzi wa TSN Farough Baghozah alisema...
Tanzania Sisi Nyumbani - TSN mteja ni haki yake kupata kilichobora
katika kiwango cha kimataifa.
"Hii
ni hatua nyingine kubwa ya kuhakikisha Watanzania wanapata vitu fresh..
kutoka nyumbani. .tena kwa bei nafuu...TSN tunahakikisha Watanzania
wanafurahia mazao yao wenyewe...tena kwa bei ya gengeni katika
Hypermarket hii.... karibuni sana TSN Hypermarket Mwanza." alisema.
Naye
waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage ambaye ndiye alikuwa
mgeni rasmi katika ufunguzi huo aliipongeza hatua iliyochukuliwa na TSN
katika kuthamini mchango wa wawekezaji wa nyumbani.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni