TAZARA BADO HALI TETE,YAKABILIWA NA CHANGAMOTO HIZI,SOMA HAPO KUJUA
SHIRIKA la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) linakabiliwa na Changamoto za Rasilimali watu pamoja na mitaji ya fedha ambapo changamoto hizo zimepelekea shirika hilo kutofikia
malengo yake.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu
mkurugenzi mkuu wa (TAZARA) Dkt Betram
Kiswaga wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachozungumzia histori ya shirika hilo
tangu lianza kufanya kazi kwenye miaka ya 1970 ambapo kitabu hicho kimeandaliwa
na nchi ya China ambao ndio waliotengeneza reli kutoka Tanzania hadi Zambia.
Dkt Kiswaga amesema TAZARA linashindwa kwenda na
kasi ya ufanyaji kazi ambao ungeweza kuliingizia taifa mapato.
Kiswaga amefafanua kuwa kutokuwepo na rasilimali
watu wenye sifa na utaalamu kumechangia
shirika hilo kushindwa kujiendesha vizuri.
“Nina mwaka mmoja kwenye Tazara ila shirika hili
limeshiindwa kufanya kazi kama tunavyotaka kutokana kutokuwa na wataaalumu
wenye sifa huku wengi wakiacha kufanya kazi na Tazara kutokana na shirika
kutokuwa na mitaji ya fedha ambayo ingeweza kuwamudu wataalamu”amesema Dk
Kiswaga.
Hata hivyo,Dk Kiswaga amesema licha ya kukumbuna na
changamoto hizo,amedai bado shirika hilo linaendelea na kutoa huduma ya usafiri
kutoka Tanzania na Zambia huku akitoa Pongezi kwa nchi ya China kuendelea kutoa
ushirikiana kwa shirika hilo.
Naye Balozi wa China nchini LU Youqing amesema Serikali ya China itaendelea kutoa
ushirikiana kwa shirika hilo.
Amesema kwa sasa wanafahamu shirika hilo linakumbana
na changamoto jambo analodai kuwa nchi yake hatosita kulisaidia shirika hilo
katika kuzitatua changamoto hizo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni