Zinazobamba

RAIS MAGUFULI AVUNJA UKIMYA AWAJIA JUU WAFICHA SUKARI,ASEMA HAYA,SOMA HAPO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi  wa Mji wa Singida, wakati aliposimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Jijini Arusha kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Dodoma, leo Mei 6, 2016
 
 
 
Rais Magufuli ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioficha sukari ili baadae waiuze kwa bei kubwa.

Amesema wafanyabiashara hao wenye tamaa ya pesa walikuwa wakifuata sukari iliyo Expire huko Brazili   na kuileta nchini ili watengeneze faida na ndo maana serikali iliwapiga marufuku kuagiza

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiwasalimia wananchi wa Katesh, Mkoani Manyara. Rais ametoka Mkoani Dodoma leo, anaelekea Mkoani Arusha kwa usafiri wa gari.

Akiongea na mamia ya wananchi hao waliojitokeza kumlaki njiani, Rais Magufuli amewatoa hofu wananchi kuhusu uhaba wa sukari kwa kuwa tayari wako  katika mchakato wa kuagiza makontena ya sukari nje ya nchi ili kuwakabili wafanyabiashara walioficha bidhaa hiyo.

Amesema kwa taarifa alizonazo kuna mfanyabiashara alienda akanunua sukari pale Kilombero zaid ya tani 3000 na hataki kuzichukua hadi leo

Pia amesema kuna mwingine ana godauni huko Mbagala yenye tani 4000  ambazo hataki kuzitoa ili wananchi wakose sukari

Rais Magufuli amesema ameviagiza vyombo vya dola viwafuatilie ili ikithibitika sukari waliificha basi ichukuliwe na kugawiwa bure kwa wananchi na pia watapigwa marufuku kufanya biashara yoyote hapa nchini

Hakuna maoni