Zinazobamba

MRITHI WA MAKONDA KINONDONI AFICHUA MADUDU TENA,SOMA HAPO HAPO


Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi akizungumza na Waandishi wa habari




“Ni nafuu ya shetani kuliko watumishi hewa hawajali shida za watu wengine, hawajali maslahi ya wengine, wewe unahangaika wao wanaishi maisha ya ajabu, ndio maana nataka hao nilale nao mbele naomba mnisapoti,najua bado wapo na wako kwenye maeneo yote,”hiyo ni kauli ya Rais Magufuli katika siku ya wafanyakazi Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika mkoani Dodoma.

Hivyo suala hilo limeazidi kuchukua sura mpya katika Halmashauri ya Wilaya Kinondoni baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Ally Salum Hapi kutangaza kuwa watumishi hewa wameongezeka na kufikia 103 ambapo hapo awali walikuwa 89, huku ongezeko hilo la watu 14 limeitia hasara serikali ya Milioni 120, huku 8 wakiwa ni walimu wa shule za Msingi, 3 walimu wa Sekondari na watatu waliobaki wakiwa ni watumishi wa Afya.

Katika hatua nyingine Hapi, ameeleza kuwa Halmashauri ya kinondoni inajumla ya watumishi 9000, hivyo katika hao watumishi hewa 103, watumishi 16 wameanza kurejesha pesa na kufikia milioni 94 na kusisitiza bado wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wengine.

Pia ameongeza kuwa licha ya kuwabaini watumishi hewa wilaya yake inaendelea na operesheni safisha Kinondoni ambayo imeadhimia kuondoa uhalifu wa aina yeyote katika wilaya hiyo ikiwemo ukwepaji kodi,kufanya biashara bila leseni, ambapo wamefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani machangudoa 52,wazurulaji 10,wapiga debe 7, na vibaka wanne.

Hakuna maoni