CHAMA CHA CUF CHAFICHUA SIRI NZITO YA UBAGUZI NA CHUKI UNAOENDELEA ZANZIBAR,SOMA HAPO KUJUA
UKANDAMIZWAJI wa demokrasia unaofanywa na serikali
ya awamu ya tano ndiyo chanzo cha ubaguzi na chuki iliyopo miongoni mwa
wananchi wa visiwani Zanzibar, anaandika Regina Mkonde.
Hayo yamesemwa leo na Twaha
Taslima, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Katika
matukio ya kukanyaga demokrasia madhara yake ni kujenga chuki na ubaguzi kwa
watanzania dhidi ya serikali yao na kwamba hali hii itasababisha vurugu na
kuathiri maendeleo ya nchi kutokana na uwepo wa muendelezo wa chuki,” amesema
Taslima.
Taslima
amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inaonesha dhahiri kwa matendo yake
kwamba haina mpango na haitaki demokrasia na kwamba mkakati wake ni
kuendelea kukandamiza demokrasia.
“Serikali
inadhani kuwa kuendelea kukandamiza kutasaidia wao kubaki madarakani zaidi na
zaidi jambo ambalo wanajidanganya,” amesema.
Licha
ya ukandamizwaji wa demokrasia, Taslima amesema CUF imeshuhudia
ukandamizwaji wa haki ya wananchi ya kupata habari na kuhabarisha kutoka na
kwamba wanahabari wanatishwa na kukandamizwa wasitoe taarifa kwa uhuru.
“Mfano
mzuri ni kutekwa kwa Salma Saidi, mwandishi wa DW Zanzibar, na kile kitendo cha
wananchi kuziwa kupata taarifa wanazopaswa kupata kama vile kuundwa na
kutekelezwa kwa sheria kandamizi ya matumizi ya mtandao,” amesema.
Aidha,
amesema kuzuiliwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya bunge hatua iliyofanywa na
serikali ya awamu ya tano imelenga kuficha wananchi shughuli zinazofanywa na
wawakilishi wao.
Kuhusu
kauli iliyotolewa na Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu akiwa London nchini Uingereza
baada ya kuulizwa swali kuwa kwa nini serikali ya awamu ya tano hairushi
matangazo ya bunge live.
Na
kujibu kuwa sababu ni watanzania kutopenda kufanya kazi wakati wa matangazo
hayo yanaporushwa kwa kuwa hupoteza muda wao kuangalia bunge, Taslim amemtaka
Waziri kuomba radhi watanzania.
“Waziri
Mkuu bila aibu alisema kuwa wataznaia hawapendi kazi na wanakuwa wanaangalia
bunge muda wote badala ya kufanya kazi, hii kauli ni ya kidhalilishaji sana kwa
watanzania,” amesema.
Taslima
amesema hiyo siyo hoja kutokana n akwamba kama watanzania wangekuwa wanaangalia
bunge live muda wote maendeleo na maisha yao wengi yangekwama.
“Si
kosa wananchi kufuatilia bunge kwa kuwa mwananchi yeyote makini anafuatilia
taarifa za masuala mbalimbali ya nchi kwani maamuzi yanayojadiliwa na kuamuliwa
bungeni yanaathiri maisha yao pia inatoa mwanya kwa wananchi kupima serikali yake
kama inatekeleza majukumu yake,” amesema.
Amesema,
serikali ni lazima ikaangalia upya na kufuata misingi ya demokrasia , haki za
wananchi kwa sababu haki inaponyimwa husababishwa kutoelewana baina yao.
“Serikali
kazi yake kubwa hivi sasa ni kutaka kuwarudisha nyuma wananchi kwenye uwoga wa
kutoiwajibisha serikali eti kwa kisingizio cha hapa kazi tu, aweamu ya tano
inakuja na slogan ya hapa kazi tu ya kuua demokrasia,” amesema
Hakuna maoni
Chapisha Maoni