WANAHARAKATI WAANZA MCHOKONOA MAGUFULI,SASA LHRC WAINGILIA KATI,SOMA HAPO KUJUA
STAILI ya Rais John Magufuli kutimua watumishi wa
umma kwa ‘munkari’ inawavuruga watu wengi ambapo Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC) kimeonya, anaandika Regina Mkonde.
Kabla ya LHRC kuonya, Edward
Lowassa, aliyekuwa mgombea uraas kupitia Chadema na kuungwa mkono na Ukawa pia
Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini
walionya staili hiyo na kushauri taratibu za kisheria za utumishi wa umma
zifuatwe.
Helen
Kijo Bisimba, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC ameikumbusha serikali kufuata sheria
za utumishi wa umma katika kuwawajibisha watumishi wanaotuhumiwa kufanya
makosa.
Bisimba
ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya haki za binadamu ya mwaka
2015 uliofanyika jijini Dar es Salaam, MwanaHALISI Online lilishuhudia.
“Inafahamika
kwamba, Rais John Pombe Magufuli ameikuta nchi sehemu mbaya na anahitaji
kuirekebisha.
“Ila
ni vema akafuata taratibu za kisheria wakati anapotaka kumtumbua mfanyakazi
aliyeajiriwa na serikali ambayo ndiyo anayoiongoza,” amesema Bisimba.
Anaeleza
kuwa, Rais hakuchukua uamuzi wa busara kwa kumsimamisha kazi Wilson Kabwe,
aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam mbele ya hadhara na kwamba,
alitakiwa kufanya uamuzi huo kwa kufuata sheria.
“Makonda
(Paul Makonda) hakuwa na sababu za kumsema Kabwe mbele ya hadhara, alitakiwa
afuate utaratibu, si maanishi kuwa namtetea Kabwe, bali kutokana na agizo la
rais alilotoa la kusimamishwa na kufanyiwa uchunguzi, je atakapobainika kuwa ni
msafi ataweza kumsafisha?” anahoji.
Bisimba
amewataka Watanzania waache unafiki kwamba, wapo baadhi ya wanasheria wanaojua
taratibu za kumsimaisha kazi mtumishi wa umma lakini walishindwa kumshauri
badala yake waliacha aendelee na uamuzi wake.
“Mfano
jana alikuwa anauliza wananchi, nimtumbue nisimtumbue, mbele ya hadhara, huyo
aliyekuwa anamfanyia hivyo ni mtumishi aliyeajiriwa na serikali, isitoshe Kabwe
ninavyomjua ni mgonjwa, je angepata matatizo ingekuaje?” anauliza.
Bisimba
pia ametolea mfano wa hatua iliyochukuliwa wakati wa kufukuzwa kazi Anne
Kilango Malecela, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwamba, aliju akwamba
amefukuzwa kazi baada ya kupigiwa simu akiwa ofisini.
“Kilango
alitumbuliwa wakati alipokuwa ofisini, alipigiwa simu ili kujibu baadhi ya
maswali juu ya kufukuzwa kwake, cha kustajaabisha hakuwa na taarifa kama
alifukuzwa kazi na rais,” amesema.
Amesema
kuwa, mfumo wa utumishi mbaya ulianzishwa na serikali baada ya kuuondoa mfumo
wa ujamaa na kuuweka mfumo wa ubepari.
Kwa
upande wa sheria anasema, zipo nzuri ila nyingi kati ya hizo zinahitaji
maboresho na kwamba, inahitajika Katiba Mpya ili ifanyike marekebisho ya sheria
zilizoachwa na mkoloni.
Aidha,
ripoti iliyotolewa leo inaonesha kuwa, uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba
2015 ulikuwa huru japo kulikuwa na wasiwasi wa kutokuwa na haki kutokana na
madai ya kuibiwa kura.
Ripoti
hiyo inabainisha kuwa, kwa mujibu wa uangalizi uliofanywa na LHRC umebaini
kuwa, elimu ya uraia haikutolewa vizuri, watu wenye ulemavu walipata shida
kufika maeneo ya kampeni na kutumika kwa vifaa vya serikali wakati wa kampeni
hasa magari pamoja na uchelewashaji wa kutangaza matokeo katika vituo
mbalimbali.
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni