MEYA WA UKAWA KINONDONI APATA MASAADA KUTOKA NCHINI PAKISTANI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Boniface Jacob |
BONIFACE Jacob, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni leo amepokea msaada wa dawa za binadamu kutoka kwa Jeshi la Maji la
Pakstani kupitia ubalozi wake nchini,
Akizungumza na waandishi
jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea msaada huo Jacob amesema, kikosi
hicho kilicho na watu zaidi ya 300 kimetua nchini jana.
Amesema,
kikosi hicho kimekuja na meli kubwa ya kivita kutoka nchini Pakistani kwa lengo
la kufanya doria katika Bahari ya Hindi ambayo pia imepita nchini humu.
Meya
Jacob amesema, meli hiyo ya kivita hufanya doria katika nchi zote ambamo Bahari
ya Hindi imepita kwa lengo la kukomesha ujangili wa majini.
“Baada
ya meli hiyo kutua jana ndipo uongozi wake ukaamua kutoa msaada kwa Watanzania
kwa kutoa dawa za binadamu zinazotibu magojwa mbalimbali. Hatukuweza kujua
gharama yake kwa muda huu lakini tutazisambaza katika hospitali zote za Wilaya
ya Kinondoni,”amesema Jocob.
Hata
hivyo, meya amesema mbali na kupewa msaada huo pia wamezungumza mambo
mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuimarisha ushirikiano kati ya Manispaa ya
Kinondoni na nchi ya Pakstani.
“Nimefurahishwa
sana na ujio wa wageni hao pia najisikia furaha kuwa wa kwanza kutembelewa na
ubalozi huu na kupokea misaada hii kwani ni mwanzo wa ushirikiano mzuri baina
yetu,” amesema Jacob.
Naye
Amir Mohammad Khan, Balozi wa Pakistani amesema meli hiyo ina miaka mitatu sasa
tangu ianze safari yake ya kutembea kwenye Bahari ya Hindi na hufanya hivyo
kutoa misaada kila ifikapo kwenye nchi flani.
“Tumeshatoa
misaada kwenye vituo vya kulelea yatima, shuleni na kwa watu wenye uhitaji kwa
kufanya hivyo tunakuwa tunatengeneza uhusiano mzuri kati ya nchi yetu na nchi
hizo.
“Tuna
ahidi kuongeza ushirikano baina ya Pakstani na Tanzania ili tuweze kusaidiana
zaidi kwani kuynasiku pia nchi yetu itahitaji msaada kutoka kwenu,” amesema
Khan
Hakuna maoni
Chapisha Maoni