Zinazobamba

MAASKOFU WAINGILIA KATI MGOGORO WA ZANZIBAR,WAMUONYA MAGUFULI NA CCM YAKE,WASEMA HAYA,SOMA HAPO KUJUA


Askofu Dk. Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
Askofu Dk. Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania



MTIKISIKO wa hali ya kisiasa Zanzibar umebisha hodi katika Kanisa ambapo Jukwaa la Wakristo Tanzania limetoa onyo, anaandika Pendo Omary.
Viongozi wa wa Dini ya Kikristo kupitia Jukwaa la Wakristo Tanzania kwenye taaifa waliyoitoa leo, wametuhumu Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kushindwa kukabiliana na mkwamo wa kisiasa visiwani humo.
Wamesema, udhaifu wa kikatiba uliovumiliwa kwa muda mrefu bila kutatuliwa ndio chanzo kikuu cha sintofahamu visiwani humo na kusababisha wananchi kuishi kwa mashaka.
Jukwaa hilo limefikia hatua hiyo wakati ambapo hali ya kisiasa visiwani humo ikiendelea kuyumba kutokana na matukio yanayoonesha kuanza kwa uvunjwaji wa maani.
“Sisi viogozi tunafadhaishwa na hali ya Zanzibar kwa sasa. Hali ya Zanzibar isingefikia hapo iwapo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingechukua hatua ya kutatua mgogoro huu,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Askofu Justice Ruwa’ichi.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba, upungufu uliopo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio unaosababisha kushindikana kutatuliwa kwa matatizo ya Zanzibar.
“Hata hivyo udhaifu huu wa katiba ya Muungano hauondoi wajibu wa Serikali ya Muungano kuhakikisha haki na amani vinatawala Zanzibar,” ameeleza kwenye taarifa hiyo.
Ameeleza, serikali na taasisi zinazosimamia suala la uchaguzi wanapaswa kuhakikisha uhuru, haki na amani Zanzibar zinalindwa na kuheshimiwa.
Pia wameshauri kwamba, “mchakato wa Katiba Mpya ya wananchi (Rasimu iliyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba) urejeshwe ili kuondoa utata wa serikali ya Jamhuri ya Muungano kushiriki masuala ya Zanzibar.

Hakuna maoni