FREEMAN MBOWE APONGEZWA KILA KONA,NI KWA UTEUZI WA KATIBU MKUU MPYA,WASOMI WAMVULIA KOFIA MBOWE,SOMA HAPO KUJUA
Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema |
DAKTARI Vicent
Mashinji ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) na kupitishwa na Baraza Kuu la Chadema, katika kikao chake kilichokaa
jijini Mwanza, anaandika Mwandishi Wetu.
Katika Kikao hicho cha Baraza Kuu,
Freeman Mbowe alitangaza jina la Dk. Mashinji na kuungwa mkono na wajumbe
wa baraza hilo, hivyo anajaza nafasi iliyoachwa na Dk. Willibrod Slaa,
aliyejienguwa ukatibu mkuu wa chama hicho.
Jina la Dk. Machinji halikuwa miongoni mwa wanachama wa Chadema
ambao walikuwa wanatarajiwa kumrithi Dk. Slaa kwani waliokuwa wanatabiriwa
kukatia kiti hicho ni Salum Ally Mwalimu, Frederick Sumaye, Benson Kigaila,
John Mnyika, Dk. Marcus Albanie na Prof. Mwesiga Baregu.
Nafasi ya Katibu wa Chadema ilikuwa wazi tangu Dk. Slaa
alipoondoka Chadema muda mfupi baada ya chama hicho kumpitisha Edward Lowassa
aliyetokea CCM kuwa mgombea urais wa chama hicho na kuungwa mkono na vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
WASOMI WANENA
Wakizungumza na Fullhabari wasomi na wachambuzi
mbalimbali wamemzungumzia Katibu hyo mpya kuwa ni mtu mwenye maono na
atakayeweza kuijenga chadema kisasa kutokana na elimu yake.
Hamad Mrisho ni Msomi wa masuala ya siasa kutoka
Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania amesema Kiendo cha Mbowe kumteua Katibu huyo ni
njia bora ya kukijenga chama kimataifa.
‘Kusema kweli nimeanza kumchua Mbowe kuwa ni
wanasiasa wenye uelewa mpana sana,kwani Dkt Visent ni mtu mchapakazi tena mimi
namjua sana Tangu akisoma hapa Open,naimani sasa Chadema itajengwa kisasa na
inaweza ikafanikiwa kuchukua Dola 2020”amesema Mrisho
Wasifu wa Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vincent
B. Mashinji
Professional experience
Clinical Advisor & TB/HIV lead
UMSOM-IHV
July 2008 – Present
ART Program Doctor/IMA team lead
IMA Worldhealth
August 2006 – June 2008 (1 year 10 months)
Medical Officer/Anaesthesiology
Regency Medical Centre
October 2005 – August 2006 (10 months)
Medical Officer
Muhimbili National Hospital
August 2003 – October 2005 (2 years 2 months)
Research Assistant
Freelance
November 2002 – August 2003 (9 months)
Intern Docor
Muhimbili National Hospital
September 2001 – October 2002 (1 year 1 month)
Education history
Open University of Tanzania
PhD
August 2010 – Present
AMREF/UCLA Anderson School
MDI Certificate
April 2010 – April 2010
Blekinge Institute of Technology
MBA
September 2007 – March 2010 (2 years 6 months)
UMSOM-IHV
IPEP Certificate
May 2008 – May 2008
Evin School of Management
Certificate in CSR
October 2005 – October 2005
Muhimbili University College of Health Sciences
MMed/Anaesthesiology
September 2003 – April 2005 (1 year 7 months)
Muhimbili University College of Health Sciences
Certificate in Research Methodology
September 2004 – September 2004
Makerere University
MBChB
October 1995 – July 2001 (5 years 9 months)
Mzumbe High School
ACSEE
July 1992 – June 1994 (1 year 11 months)
St. Pius X Seminary, Makoko
GCSEE
January 1988 – October 1991 (3 years 9 months)
Iligamba Primary School
Leaving Certificate/Primary School
January 1981 – October 1987 (6 years 9 months)
Hakuna maoni
Chapisha Maoni