Zinazobamba

WANAHARAKATI WA TNGP WAMKOSOA RAIS MAGUFULI,NI KWENYE SUALA LA UTEUZI WA KIJINSIA,SOMA HAPO KUJUA

Mkurugenzi mtendaji wa TGNP LILIAN LIUNDI akifafanua jambo mbele ya wanahabari mapema leo katika mkutano huo ambao ulikuwa unalenga kuzungumzia siku 100 za Rais Magufuli tangu aingie madarakani
NA KAROLI VINSENT
Wanaharakati wa maswala ya jinsia nchini Tanzania wametilia shaka  ushiriki wa wanawake katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ikiwa ni siku mia moja za uongozi huo ambapo wamehoji kushushwa kwa kiwango cha wanawake waliochaguliwa katika sehemu muhimu za maamuzi katika serikali,
Katika mkutano wa wadau mbalimbali wa jinsia uliondaliwa na mtandao wa jinsia nchini TGNP  na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam ambao mkutano huo uliokuwa na lengo la kujadili siku mia moja za uongozi wa awamu ya Tano, baadhi ya wanaharakati wamepongeza kasi aliyoanza nayo ,
  Raisi wa Tanzania DR JOHN POMBE MAGUFULI hasa katika hatua yake ya kupambana na ubadhilifu na kutaka kurudisha rasimilimali kwa wananchi wenyewe jambo ambalo wamelitaja kuwa ni moja kati ya mambo ambayo yalikuwa yanapiganiwa na wanaharakati mbalimbali nchini kwa miaka mingi iliyopita.
Kwa upande wake  mkurugenzi mtendaji wa TGNP mtandao bi. LILIAN LIUNDI ameonyesha masikitiko yake katika uteuzi wa Rais Magufuli kwenye Baraza la mawaziri akidai haujazingatia uwiano wa kijinsia
Bi Liundi amefafanua kuwa  kati ya mawaziri na manaibu waziri 35, wanawake ni Tisa sawa na asilimia 25.7 huku wanaume wakiwa 26 sawa na asilimia 74.28 ,hivyo hivyo katika uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu haujazingatia usawa wa kijinsia.

Mkurugenzi mtendaji huyo wa TGNP ameongeza kuwa katika uteuzi unaotarajiwa wa ukuu wa Mkoa na Wilaya wametaka Rais ni ni vyema  akazingatia usawa wa kijinsia  kwa mdai kuwa  nchi imesaini mikataba na matamko mengi ya  usawa kijinsia ya kimataifa.

 
Pichani ni Prifesa Meena akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku 100 za Rais magufuli akiwa madarakani 

Hata hivyo mwenyekiti wa mtandao wa wanawake na katiba Profesa RUTH MEENA ambaye alijumuika katika kongamano hilo ametoa wito kwa rais na makamu wake kuweka mfumo wa uwajibikaji ili kuondoa mfumo uliopo sasa ambao ameufafanisha na wa kikoloni.
 Waharakati mbali mbali wa mambo ya Kijinsia wakijadili siku 100 za Rais Magufuli Tangu aingie madarakani

Hakuna maoni