BREAKING NEWS,MAJIPU YATUMBULIWA TENA LEO,WAKURUGENZI WANNE WASIMAMISHWA KAZI,RUNGU PIA LATUA OFISI YA CAG,SOMA
Pichani ni Waziri nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane |
NA KAROLI VINSENT
WAZIRI nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na
serikali za mtaa,George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne ambao
ni Elizabeth Chitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera,
Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni
Mtwara, Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita, baada ya kubainika wakurugenzi hao wametenda kosa la kuwahonga wakaguzi wa fedha kutoka katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) ili wapewe hati safi huku Halmashauri hizi zikiwa na ufisadi .
Pia, Waziri Simbachawene amemsimamisha
kazi mkurugenzi Halmashauri ya Tunduma Mkoani
Mbeya Bi Halima Ajali ili kupisha
uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka.
Hata hivyo
Waziri Simbachawane pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa
ofisi ya mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini,CAG waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe hati safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na
ubadilifu wa fedha za Umma.
Akizungumza na waandishi wa habari mda huu Jijini
Dar es Salaam,Waziri Simbachawene amesema Wakurugenzi hao wamegundulika baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na
wizara yake,
Waziri Simbachawene ameyataja makosa yao kila mmoja wao
ambapo amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi, Bi Chitundu ametenda ametanda kosa baada ya kumwagiza mweka hazina wake Majaliwa Bikwato atoe rushwa
ya Milioni tatu kwa maafisa ya (CAG) kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo ,
Ambapo Maafisa hao wa CAG waliopeka pesa hizo ni Stevin Buawa,John
Elias pamoja na Kilembi Mkole,
Waziri Simbachawene amesema Katika Halmashauri ya Nanyumbu
ambapo ameidai tarehe 26 Juni 2015
mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel
Mugesa wamlimkabidhi fedha ya Milioni 3 na laki tano afisa wa CAG ambapo afisa huyo alipokea pesa hizo kwaniaba
ya wenzake kwa lengo la kutoa hati safi,
Sanjari na
huyo pia Waziri Simbachawene amesema hata katika Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita ambapo amedai mwezi Novemba mwaka jana , Mkurugenzi wa Halmahsauri
hiyo Abdalla Mfaume na mweka hazina wake wamliwapat ia fedha maafisa wakaguzi wa
C AG ambao walipokea rushwa ya milioni 16 ili wafiche ufisadi walioubaini,
Hata hivyo Simachawene amesema katika Halmashauri
hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa ukiwemo malipo ya mishahara
hewa pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadhi ,
Aidha,Waziri Simbachawene amesema katika wilaya hiyo
ambapo mkaguzi wa mkoa wa Geita alipewa
Rushwa kutoka kwa viongozi wa wilaya
hiyo ili kuficha ufisadi wa milioni 90 ambazo zilitengwa kwa ajili ya kununulia
dawa.
Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene amesema Kwa mamlaka aliyekuwa nayo amemasiamisha
kazi pia mkurugenzi wa Mji wa Tunduma Bi Halima Ajali baada ya kubainika kutumia vibaya
madaraka aliyokuwa nayo.
Amesema Mkurugenzi huyo alikuwa anawatumia watoto
wake kwenye shughuli za Halmashauri huku akiwalipa pesa pamoja na kuikosesha mapato
Halmashauri hiyo yaliyotokana na
Ushuru wa Magari kwenye Mpaka wa Tunduma,
Vilevile waziri Simbachawene amemteua Erick Mpunda kukaimu nafasi ya mkurugenzi
huyo ambapo Mapunda kabla ya kuteuliwa kwake hapo alikuwa Mkuu wa Rasilimali watu
wmkoani Mbeya.
Waziri Simbachawene amemuagiza Katibu kongozi
kuwasimamisha watendaji wote ambao walihusika na rushwa hizo kwenye ofisi ya CAG kwa madai kuwa wapo kwenye Mamlaka yake,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni