WAENDESHA PIKIPIKI KUTOKA NCHINI URUSI AMBAO WAMETEMBEA NCHI ZAIDI YA 30 AFRIKA KUHAMASISHA UTAMADUNI WAO HABARI KAMILI HII HAPA,SOMA HAPO KUJU
Wa Kwanza kushoto ni Iurii Volkav ambaye ni mwendesha pikipiki kutoka nchini Russia akifuatia katikati ni Mwandishi wa kituo cha Eatv pamoja na kulia niIlia Dubinni ambaye naye ni mwendesha pikipiki
NA KAROLI VINSENT
KATIKA kuhakikishwa wanaeneza tamaduni wa nchi ya Urussi katika bara za Afrika,Wananchi wawili kutoka nchi hiyo wamezunguka
katika nchi 30 za bara za afrika kwa kutumia usafiri wa pikipiki ili kueneza
ujumbe mbali mbali.
Hayo yamesemwa leo Jijini dare s Salaam, Iurii Volkav
na Ilia Dubinni ambao ndio waendesha pikipiki kutoka nchini Urusi wakati wa
mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini,ambapo Volkaov
akizungumza kwa niaba ya Mwenzake amesema matembezi hayo katika bara la afrika
yanalenga kuhamisisha nchi za kiafrika kuiga mfano wa umoja na mshikamo uliopo
katika nchi yao,
Amesema Umoja huo katika nchi yao umechangia kuinua
sekta mbali mbali huku akitolea mfano sekta ya teknolojia ambapo amedai
imechangiwa zaidi na umoja huo,
Volkav amesema sanjari na kuhumibiri umoja katika
nchi yao pia amesema matembezi hayo yamebeba na dhana ya kuzitaka nchi za
kiafrika kuwa na utamaduni wa kuwa na ubunifu kama unaoendelea kufanyika nchini
mwao ambapo wanautaalumu wa kwenda mwenzini huku akitaka nchi za kiafrika kuiga
jambo hilo.
Ameongeza kuwa Utaalamu huo wa haujaumbiwa katika nchi ya Urusi pekeyao huku
akitaka nchi za Kiafrika kujitosa katika teknolojia hiyo kwa madai kuwa kila
mtaaluamu anaweza kufanya hivyo,
Volkav amesema Licha ya kufika Tanzania
amependezeshwa na ukarimu uliopo nchini huku akifarijika na vivutio vya utalii
vilivyopo,
Hata hivyo amesema ziara hiyo itafanyika zaidi ya
nchi 60 zilizopo bara la Afrika huku mpaka sasa ametembea nchi 30.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni