Zinazobamba

TAKUKURU YAJAA MAJIPU,WAZIRI KAIRUKI AWABANA,SOMA HAPO KUJUA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgi13V-kR7g-xiYv7vFM-u0yiADVjWsOSclwuaZ7gJD6fI-fi9iQ6kYUNlNd-t5FBr98oh2O5skdp5mDFse6I0Hrj0IH6fYxMU5KbTave2j2xZljfSLwRy5vYu83ZRrWXT0ReBVruuEA5UQ/s1600/DSC03400.JPG


WAZIRI wa Nchi, Ofisi Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki  amesema kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ina baadhi ya watendaji wametumia nafasi zao vibaya na kufanya chombo hicho kukosa uaminifu  hivyo na kufanya chombo hicho kuwa na ‘majipu’ ambayo yanatakiwa kupasuliwa.
Angela ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa utendaji kazi wa Takukuru uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema  chombo hicho ni muhimu lakini kuna baadhi wametumia nafasi zao vibaya katika kufanya kazi na taarifa anazo hivyo atashughulikia ikiwemo na kuandika kiapo cha mali zao na kama walifanya warudie kujiridhisha.
 Amesema kuwa Takukuru inatakiwa kufika wilayani na mikoani kutokana na fedha nyingi za miradi ya serikali zinakwenda huko ambapo ameutaja mkoa wa Kilimanjaro  unawatendaji ambao wametumia madaraka vibaya wa ubadhirifu wa fedha za serikali hivyo Takukuru lazima ichukue hatua dhidi yao.
Amesema kuwa ikitokea kuwepo na  kutowajibika kwa chombo hicho serikali iamweza kuwandoa wote kutokana na kuwepo kwa watu wenye sifa wa kufanya kazi hiyo.

Aliongeza kuwa katika Takukuru inatakiwa kujiridhisha na uchunguzi na  sio kuwa idadi nyingi za kesi ambazo mwisho wa siku kesi hizo wanashindwa kutokana kuushindwa  kuwa na uchunguzi wenye ushahidi.
Aidha amesema kuwa baadhi ya mahakimu watakosa kazi kutokana na baadhi ya kesi wameendesha kwa kupindisha na kuwapa  washitakiwa haki wasio kuwa nayo.

Waziri Angela amesemaTakukuru wafanye kazi kwa waadilifu kwa kuwalinda watoa taarifa ili waendelee kutoa taarifa kwa watu wanaojua kuwa wanahujumu nchi kwa kutumia madaraka yao.
Amesema watumishi wa Takukuru wana masilahi mazuri kuliko wa wafanye kazi wengine ikiwa ni kuwaondoa katika ushawishi wa kuwa na tama kutokana unyeti wa chombo hicho.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishina (CP), Valentino Mlowola amesema wameokoa sh. Bilioni Saba (7) ambazo zilikuwa ziingie kwenye mifuko ya wabadhirifu wachache ambao wanatumia nafasi zao vibaya kwa masilahi yao.
Amesema walipokea malalamiko 4,675, uchunguzi uliokamilika wa majalada hayo ni 667, majalada yaliyokwenda kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), ni  278,   majarada yaliyorejeshwa na DPP, ni 172 kwa ajili ya  vibali vya kufungua mashitaka  na kesi mpya 314 nchini kote, na kesi zilizoshinda 132 ambao wamefungwa na wengine kulipa faini.

Hakuna maoni