RUNGU TRA KUWAANGUKIA MC WA SHEREHE,WAPAMBAJI NA DJ,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mkurugenzi wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi wa (TRA),Richard Kayomba akizungumza na waandishi wa habari h |
NA KAROLI VINSENT
KATIKA
kuhakikisha inapata vyanzo vya Mapato ,Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ipo
mbioni kuanza kukusanya kodi kutoka kwa
washereheshaji wa sherehe mbali mbali ,wapambaji wa sherehe hizo pamoja
wapiga muziki (Ma DJ).
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi wa Huduma na elimu kwa mlipa wakodi wa (TRA),Richard Kayomba wakati
wa mafunzo ya wadau hao,ambapo Kayomba amesema
semina hiyo imekuja na mwamko kutoka kwa shereshaji hao ambapo alitaka
kupata elimu kutoka TRA ili waweze kulipa kodi.
Amesema TRA ilipokea kwa kauli moja mwitoko huo kwa
madai kuwa kwa sasa wao wanatafuta vyanzo vyengine vya mapato ili kuhakikisha
wanaongeza mapato kwa serikali.
Amsema watu wanaofanya shughuri hizo wamekuwa
wakipata fedha kutoka kwa wateja wao huku TRA ilikuwa haipati fedha zinazotokana na kodi,
Mshereheshaji Rukia Mtingwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Faida ya wao kulipa kodi |
Kayomba amefafanuwa kuwa mara baada ya semina hiyo
na wadau hao ,TRA watawawekea njia
ambayo itakuwa rafiki itakayowawezesha kulipa kodi kwa urahisi jambo
analodai litachangia kuboresha maisha ya Mtanzania,
Kwa upande wao washereheshaji wamesema kitendo cha
wao kuanza kulipa kodi ni jambo jema ambalo wanaliona litachangia kuibadilisha
maisha ya Watanzania ambayo matumizi hayo ya kodi yataelekezea kuboresha huduma
kwa jamii.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni