CHUO HICHI CHAKWENDA NA MAJI,TCU YAKIFUNGIA RASMI,SOMA HAPO KUJUA
IKIWA ni siku 10 kupita baada ya mtandao huu
kuripoti mgomo wa walimu katika Chuo cha Kimataifa cha Tanzania (TIU) kilichopo
Kimara Stop-Over, Dar es Salaam, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imekifutia
leseni chuo hicho, anaandika Faki Sosi.
Walimu hao waligoma kuingia
darasani kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na kutolipwa malimbikizo ya mishahara
yao pamoja na kutopewa mikataba ya kazi.
Taarifa
iliyotolewa na Profesa Yunus Mgaya, Katibu Mtendaji wa TCU kwa vyombo vya
habari imeeleza kuwa, chuo hicho kimefutiwa leseni yake kutokana na kushindwa
kutimiza masharti yaliyobainishwa kwenye leseni iliyowepewa.
Mgaya
ameleza kuwa, chuo hicho kimeanzisha kufundisha programu za astashahada na
stashahada bila ithibati ya mamlaka husika na kuongeza TCU haitambui program
zinazotolewa na chuo hicho
Hakuna maoni
Chapisha Maoni