RUNGU LA MAGUFULI LATUA KWENYE VYUO VIKUU,TCU YAIBUKA NA KUVIFUNGA VYUO VIKUU HIVI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Katibu mtendaji wa (TCU)Profesa Yunus Mgaya |
NA KAROLI VINSENT
TUME ya Vyuo vikuu nchini (TCU) imekifutia kibali kilichoanzisha vyuo vikuu wiwili
vishiriki vya St Joseph University of Agricultural science and Tecnology
(SJUCAST) na St Joseph University College of iformation Technology (SJUCIT) vilivyo Kampasi ya Songea ,vyuo hivyo ambavyo
vinamilikiwa na Kanisa katoliki nchini.
Hata hivyo,TCU pia imeidhinisha kibali kwa wanafunzi
wote wanaosoma Vyuo hivyo kupata ruhusa
ya kuhamia vyuo vyengine ambapo watasoma kwa gharama zinazotokana na vyuo hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mda huu jijini
Dar es Salaam,Katibu mtendaji wa (TCU)Profesa
Yunus Mgaya amesema kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha sheria ya vyuo
vikuu,sura ya 346 ya sheria Tanzania inatoa Mamlaka ya tume hiyo kusimamia na
kudhibiti ubora wa vyuo vikuu nchini,
Profesa Mgawa ametaja makoa yaliopelekea vyuo vikuu
hivyo kufungia ni baada ya kuwepo kwa mlolongo wa matatizo ya ubora wa chuo,Uongozi mbovu
pamoja na ukiukwaji wa sheria na taratibu za uendeshaji wa chuo kikuu.
Amesema baada
ya uamuzi huo wakuvifungia vyuo hivyo,amewataka wanafunzi wote 2046 wa SJUCAST na SJCIT wanataarifa kuwa watahamishiwa kwenye vyuo
vikuu vingine ambavyo vinafundisha
program za masomo zinazofanana na masomo wanayosoma hivi sasa,
Ameongeza kuwa wanafunzi wote wanapaswa kuondoka
chuoni hapo mara moja baada ya kukamilisha taratibu za kukabidhi
mali na vifaa vyengine vya chuo kwa mujibuwa wa sheria
Profesa Mgawa amefafanua kuwa wanafunzi wote
wanatakiwa kuripoti kwenye vyuo watakapopangiwa wakati wa kufunguliwa kwa
muhula(semester) wa pili, huku kwa wale
wanafunzi wanaonufaika na bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu juu,mikopo yao itahamishwa katika vyuo watakavyohamishiwa,
Vilevile Profesa Mgawa amevitaka vyuo vyote vikuu
nchini kufuuta sheria na kuzingatia
utoaji wa elimu inayokidhi viwango vya ubora wa kimataufa, huku akidai kuwa
tume haitasita kukichukulua hatua chuo kikuu chochote kitakachokiuka kanuni
hizo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni