Zinazobamba

MSAFARA WA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA WAPOPOLEWA,WAFANYAKAZI WA MSD WAFUNGA BARABARA,USALAMA WA TAIFA NA POLISI WAZIDIWA NGUVU,SOMA HAPO KUJUA


MSAFARA wa Waziri mkuu, Kassim Majaliwa umekumbana na nguvu ya wananchi pale uliposimamishwa  na wafanyakazi wa Bohari ya kuhifadhi dawa (MSD) walipomtaka asimame ili wamweleza shida wanazokumbana nazo kutoka kwenye eneo lao la  kazi.Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Tukio hilo la aina yake limetokea leo Jioni maeneo ya Bohari ya MSD yaliyoko Mabibo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam,mara  baada ya Waziri mkuu alipomaliza kupokea msaada wa Vifaa mbali mbali  vya Hospitali kutoka kwa muungaiko wa Kampuni za vinywaji nchini,

Ambapo kwa mujibu wa Mwandishi wa Fullhabari.blogs aliyekuwepo eneo hilo amesema hali ya hiyo ilianza kutokea kabla ya Waziri mkuu ajafika eneo hilo ambapo anaeleza kuwa kundi la wafanyakazi wa Bohari hiyo walikuwa wamekusanyika huku wakibeba mabango mbali mbali yenye ujumbe wa kueleza mambo wanayofanyiwa Boharini hapo,


Wafanyakazi wa MSD wakifunga barabara wakimzuia waziri mkuu asipite


 Maafisa Usalam wa Taifa wakimweleza Waziri mkuu kuhusu hali ilivyo kuhusu wafanyakazi hao
 WAZIRI mkuu Kassim Majaliwa naye akijalibu kuwatuliza wafanyakazi hao mara baada ya Usalama wa Taifa kushindwa kuwatuliza
 Sehumu ya Bango kwa waziri mkuu
 Mmoja wa Wafanyakazi akiongea kwa niaba ya wenzake akimweleza waziri mkuu matatizo yao
 Polisi wakijaribu kutuliza fujo kutoka kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho,


 Waziri mkuu akizungumza na wafanyakazi hao


Msafara wa Waziri ukiruhusiwa mara baada ya kuwasikiliza wafanya kazi hao


   Habari kamili inaendelea


Wakati Waziri mkuu akiwa anakaribia kufika eneo hilo Mtandao huu ulishuhudia watu wanadaiwa kuwa ni Maofisa Usalama wa Taifa walikwenda kwa wafanya kazi hao na kuwapora Mabango hayo yalikuwa yanaeleza ujumbe huo, usalama hao walifanya hivyo ili waziri mkuu asiyaone ,
Mara baada ya maofisa hao wa usalama kuwapora na Mabango hayo  ambapo walifanikiwa huku  jambo hilo lilowachukiza wafanyakazi hao,huku baadae kidogo waziri mkuu akafika eneo hilo na kwenda moja kwa moja kwenye upokeaji  wa vifaa vya hospitali  kutoka kwenye Kampuniza vinywaji nchini wa vifaa  hivyo ambayo vyenye thamani ya Bilioni 20,
Aidha,Wakati Waziri mkuu akimaliza zoezi  hilo la kupokea vifaa na kuanza kuondoka na msafara wake,ndipo songombingo likaanza  baada ya kundi la wafanyakazi walipotanda na kufunga  barabara ya kutokea kwenye eneo hilo na kumzuia waziri mkuu asiendoke,
Licha ya Wafanyakazi hao kuzuia msafara huo,maofisa wa usalama wa Taifa ambao walikuwa wanamlinda waziri mkuu pamoja na Jeshi la Polisi walijitahidi kuwazuia wafanyakazi hao jambo lilokuwa ngumu kutokana na nguvu ya wafanyakazi hao,
Pia hali  hiyo ikamfanya Waziri mkuu kushuka kwenye Gari na kwenda kuwasikiliza wafanyakazi huku wafanyakazi hao wakiimbia nyimbo mbali mbali  ikiwemo
 “Waziri mkuu tumechoka tumechoka na mateso”
Ndipo waziri mkuu akawataka wafanyakazi hao wamweleze tatizo ni nini,

Akizungumza kwa  niaba ya wafanyakazi hao alimwambia waziri mkuu kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kumchoka mwajili  wao kwa hatua yake ya kuwalipa malipo madogo,
“Waziri mkuu tumechoka na mateso ya mwajili wetu huyo amekuwa akitulipa mshahara wa 5000 kwa siku,pesa hii ni kula mlo wa chana na chai na nauli,ukizingatia sisi tunafamilia pesa hii ni ndipo, huku akitukata pesa na mifuko ya kijamii lakini hapeleki pesa hizo,"
"Pia waziri mkuu tunafanya kazi kwa saa 12 huku tukiteswa,tunakuomba waziri mkuu tunajua serikali ya awamu ya tano ni serikali ya wanyonge naimani utaweza kutusaiodia sisi wanyonge”amesema mmoja wa wafanyakazi hao kwa niaba ya wenzake,
   WAZIRI MKUU ANENA
Akijibu hoja hizo waziri  mkuu amewataka wafanyakazi hao,kuwa wtulivu na kuwataka wamwache aende huku akisema kuwa kesho Waziri wa kazi na ajira,Jestina Muhagama na mkurugenzi wa Mfuko wa Jamii PPF atakuja kesho kuwasikiliza
“Nimewasikiliza kesho waziri wa Ajira,Jestina Muhagama atakuja hapa asubuhi pamoja na mkurugenzi wa PPF kuja kuwasikiliza madai yenu na kuyafanyia kazi,nakuomba wewe ulisema kwa niaba ya wenzako ni uandike vizuri hayo madai yenu kesho akija waziri muweleze naimani tatizo lenu litakwisha,kwa sasa hivi nawaomba niacheni niende”amesema Waziri mkuu,
Mara baada kusema wanyakazi hao walitoa kauli za furaha huku wakiimba nyimbo mbali mbali

Hakuna maoni