MOSHI KWENYE IKULU YA MAGUFULI WATAFUTIWA DAWA,MANISPAA YA ILALA YAJA NA HICHI,SOMA SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Isaya Mgurumi |
NA KAROLI VINSENT.
KATIKA kuhakikisha wanakabiliana na Moshi wa samaki
katiko soko la feri jijini Dar es Salaam ambao ulikuwa unaibuguzi Ikulu ya Rais
John Magufuli,
Hatimaye Manispaa ya Ilala imetafuta ufumbuzi wa
kadhia hiyo Mara baada ya kununua majiko 48 mapya na ya kisasa ambayo
yatatumiwa na wapishi wa samaki katika soko hilo.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Isaya Mgurumi wakati alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari ambapo amesema kwa sasa Manispaa hiyo baada ya kutambua
kadhia hiyo imenunua majiko 48 mapya ya kisasa ambayo yanatumia nishati ya
Gesi kwa ajili ya kutatua tatizo hilo.
“Majiko haya 48 ya Gesi yatatumika kwa ajili ya kupikia
wauza samaki katika soko la feri kwani matumizi haya ya jiko la gesi yatasaidia
kuondokana na Moshi mkubwa ambao ulikuwa unatoka katika soko hilo,na moshi huo
tumechunguza tumejua ulikuwa unatokana na matumizi ya mwanzo ya nisharti ya
kuni,”amesema Mgulu,
Amesema hatua ya sasa iliyobakia ni kufunga Gesi
kwenye majiko hayo pamoja na kuweka uzio wa Bati ili iweze kuwasaidia wauza
samaki hao kujikinga na mvua zinazonyesha,
Sanjari na hilo amesema kwa sasa Manispaa hiyo
imedhamilia kuweka mazingira safi katika soko hilo ili kuhakikisha wanazuia
magonjwa ya mlipuka ambayo yanayoweza kutokea kutokana na uchafu katika soko
hilo.
Katika hatua nyengine Manispaa hiyo imesema zoezi la
umoaji wa jengo la gorofa 16 kwenye mtaa wa Indira Ganji jijini hapa unaendelea
vizuri mara baada ya Manispaa hiyo kushirikiana na idara mbali mbali za serikali
kumpata mkandarasi atakaye livunja jengo hilo,
Amesema mkandarasi huyo mzawa ametokana mara baada
ya kampuni sita kujitosa kwenye ushindani wa tenda la kuvunja jengo hilo
huku,Kampuni tano zikishindwa na tenda hiyo ambapo Kampuni ya kizawa ndio iliyoshinda
tenda hiyo yenye thamani ya milioni 900.
Amefafanua kuwa katika kipindi cha siku tatu tangu
kampuni hiyo ya kuanza uvunjaji huo,teyari Kampuni hiyo imevunja gorafa tatu.
Huku akisema Kampuni hiyo imepewa siku 60 iwe imemaliza kazi ya kulivunja jengo
hilo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni