Zinazobamba

CHADEMA YAKWAA TENA KISIKI DAR,POLISI WAZUIA MAANDAMANO YAO,SOMA HAPO KUJUA



Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika hapo kesho na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuelekea Ikulu jijini Dar es salaam kushinikiza kurejeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Naibu Kamishna wa Polisi Simon Siro amesema Chama hicho kinatakiwa kutumia mbinu nyigine ya kushinikiza kurejeshwa kwa matangazo hayo ya Televisheni ya Taifa na sio kupitia maandano.

Hakuna maoni