Zinazobamba

WAHARIRI WA GAZETI LA MWANAHALISI NA MAWIO WAACHIWA KWA DHAMANA,SOMA HAPO


Mhariri wa MwanaHALISI, Jabir Idrissa (kushoto) na Mhariri Mtendaji wa Mawio, Simon Mkina wakitoka Kituo cha Polisi cha Central baada ya kuachiwa kwa dhamana
Mhariri wa MwanaHALISI, Jabir Idrissa (kushoto) na Mhariri Mtendaji wa Mawio, Simon Mkina wakitoka Kituo cha Polisi cha Central baada ya kuachiwa kwa dhamana



MHARIRI wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Mhariri wa gazeti la MwanaHALISI ambaye pia ni mwandishi Mwandamizi wa gazeti la Mawio, Jabir Idrissa wameachia kwa dhamana na Jeshi la Polisi, baada ya kutimiza masharti ya dhamana hiyo. Anaandika Josephat Isango … (endelea).
Wahariri hao waliojisalimisha jana majira ya saa tisa jioni baada ya kupokea taarifa ya kutafutwa na jeshi la polisi kwa siku tatu na kuhojiwa kwa masaa nane, lakini walipomaliza majira ya saa tano usiku walinyimwa dhamana na polisi kwa madai leo asubuhi wangepelekwa mahakamani.
Jeshi la polisi walishindwa kuwapeleka mahakamani wahariri hao, lakini walifungua dhamana kwa masharti ya kila mtuhumiwa kuwekewa dhamana ya Sh. 20 milioni, huku akitakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili.
Mkina na Jabir wametimidha masharti hayo kwa kudhaminiwa na wadhamini wawili kwa kila mmoja huku kila mdhamini akisaini bondi ya Sh. 10 milioni.
Wahariri hao wametakiwa kuripoti kituoni hapo kila siku saa mbili asubuhi mpaka hapo watakapopewa utaratibu mwingine

Hakuna maoni