SERIKALI YA MAGUFULI KUYAFUNGIA MAGAZETI HAYA,NI YALE YALIOKUWA YANAMSAKAMA LOWASSA NA MBOWE,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni mkurugenzi wa Idara ya Habari maelezo,Assah Mwambene |
GAZETI la Jambo leo na Raia Tanzania yote kwa pamoja ambayo yanatoka kwa siku, yako
mbioni kufungiwa na Serikali ya Rais John magufuli.(Mtandao huu umedokezwa).Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Ofisi ya
msajili wa Magazeti nchini,ambazo
mtandao huu umezipata zinasema kwa sasa
ofisi hiyo ya msajili itafikia uamuzi baada ya kubainika Magazeti hayo yamekiuka sheria ya
magazeti ya mwaka 1976.
Makosa ambayo yanadaiwa kufanywa magazeti hayo ni
ile ya wamiliki wa magazeti hayo kuyauza kinyemela bila ya hata
kuishirikisha ofisi ya msajili wa magazeti nchini kama sheria ya magazeti
inavyokata,pia kuchangia kuikosesha serikali mapato kutokana na uuzwaji huo .
Taarifa za magazeti hayo kuuzwa zilipotiwa wiki
mbili zilizopita kuwa,Gazeti la Jambo leo ambalo mwanzo lilimilikiwa na Kampuni
ya Jambo Concepts Tanzania ambapo
kwa sasa inadaiwa kuwa kampuni hiyo imeliuzwa Gazeti hilo kwa Kampuni ya
Quality Media Group ambayo inamilikiwa na Mwenyekiti wa Klabu ya mpira ya
Yanga,Yusuf Manji.
Mbali na hilo,Gazeti
la Raia Tanzania pia nalo limeuzwa pia kutoka kwa Bodi ya wanahisa wa Gazeti la
Raia Mwema ambapo kwa sasa Bodi hiyo imeliuza Gazeti hilo kwa Kampuni ya TSN
supermarket,inadaiwa sababu ya Bodi ya wamiliki wa Raia Tanzania kuliiuza
gazeti hilo baada ya kuporomoka kimauzo.
“Ninachokwambia magazeti haya lazima yafungiwe ndugu,maana
yamekiuka sheria ya magazeti ambayo inawataka walete taarifa ofisi ya
msajili,lakini hawa hajafanya hivyo ,tena wameikosesha mapato serikali maana
wanauziana magazeti kinyemela huku serikali haipati mapato,nakuhakikishia
lazima yafungiwe tu.”kimesema chanzo chetu kilichopo ndani ya ofisi ya msajili
wa Magazeti.
Kuibuka
kwa taarifa hizi kunakuja ikiwa ni miezi mine tangu uchaguzi mkuu kumalizika
,ambapo Magazeti haya yote katika
kipindi cha Kampeni yalikuwa yanatumika katika kueneza sera za kipropaganda kwa
kumbeba alikuwa Mgombea wa Urais kupitia chama cha mapinduzi CCM,John Magufuli
na kumshambulia –
Aliyekuwa Mgombea wa Urais kupitia chama cha
Demokrasia na Maendelea Chadema ambaye alikuwa anaungwa mkono na vyama
vinavyounda ukawa,Edward Lowassa,kwa kumwandikia makala za kumdhalilisha,
Akizungumza na Fullhabari,blogs,mwandishi wa Gazeti
la Raia Tanzania ambaye akutaka kutaja jina lake mtandaoni kwa kuhofia ajira,ameumbia
mtandao kuwa wahariri wa gazeti lake wamechangia kuliua gazeti hilo,
“Sikufichi bwana,hawa mabwana (Wahariri) wameliua
gazeti hili wenyewe,walikubali wenyewe kuiingia kwenye mkenge wa sera za CCM na
kuanza kuponda upinzani,wakawagawa wasomaji ndipo Gazeti lilipoingia kwenye
msukosuko mpaka wamiliki wakaliuza kwa bei ya kutupwa kwa hawa watu wa TSN,wamejua aliuziki
kutokana kuwa alihuziki”
Maoni 1
pls fungeni blog ya wananchi pia maana nayo ilizidi
Chapisha Maoni