Zinazobamba

KASI YA WABUNGE WA UKAWA,WAITISHA CCM,SOMA HAPO KUJUA

Baadhi ya Wabunge wa CCM wakiwa katika semina elekezi mjini Dodoma
Baadhi ya Wabunge wa CCM wakiwa katika semina elekezi mjini Dodoma
 
KASI ya wa wabunge vijana wanaotokana na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) imeionekana kuwatia kiwewe wabunge wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Hali hiyo imejionesha leo katika mji wa Dodoma kutokana na wabunge wa CCM kujifungia katika ukumbi wa mikutano wa CCM makao makuu (White House) wakipeana semina elekezi.
Katika semina hiyo iloiyogubikwa na usiri mzito huku katibu mwenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye akiwafukuza waandishi katika semina hiyo ambayo ilikuwa ikiendeshwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana.
Vyanzo vya habari kutoka katika ndani ya semin hiyo zinasema kuwa lengo kubwa ni kukabiliana na wabunge wa upinzani ambao wanaonekana kuwa na hoja nzito na za msingi.
Mbali na hilo chanzo kinaeleza kuwa Kinana kawataka wabunge wa CCM kujenga utamaduni wa kuisimamia serikali badala ya kuwa washabiki tu.
Katika hatua nyingine inaelezwa kwamba CCM imekuwa na migogoro ambayo inatokana na wabunge wake kugawanyika.
Katika semina hiyo ya siku mbili inalenga kuhakikisha wabunge wanarudisha imani kwa Watanzania ambao wanaonekana kukata tamaa na CCM.
Hata hivyo imeelezwa ajenda zilikuwa tatu ikiwa ni pamoja na nia ya kuisimamia serikali, kufanya tathimini ya uchaguzi mkuu uliopita na kujadili yaliyojitokeza katika kura za maoni.
Ili kuthibitisha kuwa kikao hicho kilikuwa na usiri mkubwa katibu wa wabunge wa CCM, Jenister Muhagama alikataa kuzungumzia mweneno wa semina hiyo kwa madai kwamba msemaji ni Katibu mwenezi huku naye Nape akidai siyo msemaji.

Hakuna maoni