DKT EDWARD HOSSEAH ATOWEKA NCHINI,AKIMBIA RUNGU LA MAGUFULI,SOMA HAPO KUJUA
MKURUGENZI wa
zamani wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Dkt Edward Hosseah
ameondoka nchini na kuibua sintofahamu.(mtandao huu umedokezwa) Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Taarifa
za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata zinasema Hosseah ameondoka nchini kwa
kile kinachoiitwa ni hofu,kutokana na utawala wa Rais John Magufuli ambao
unatajwa kujiandaa kumburuza makahamani kutokana na tuhumu lukuki zinazomwandama.
Dk
Hoseah (57) alifukuzwa kazi na Rais Magufuli tarehe 16 desemba ,mwaka huu kwa
madai ya kutoridhishwa na utendaji wa kazi yake,
Katibu
mkuu kiongozi ,Ombeni Sefue alitangaza
kufukuzwa kazi kwa Dk Hoseah kwa kile
anachodai kushindwa kuzuia rushwa, na baadaye kubainisha kuwa nafasi yake
kuchukuliwa na aliyekuwa Naibu mkurugenzi wa Takukuru ,Valentino Mlowola.
“Ninachokwambia
huyu bwana(Hoseah) hayupo nchini kabisa
ameondoka na yupo kwenye nchi moja ya ulaya huko,amefanya hivi ili
kuepuka kadhia, maana huyu naye anajua
anaweza kuwa ni jipu linalosubili kutumbuliwa na utawala wa Magufuli”kimesema Chanzo chetu.
Kuibuka
kwa taarifa hizi,za Dk Hoseah kuondoka nchini zinakuja ikiwa kuna taarifa ya
mkurugenzi huyo kutarajiwa kupandishwa mahakamani mda wowote toka sasa kutokana
na tuhuma lukuki ambazo zinamkabili
ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka na kushindwa
kuzibiti rushwa nchini,
Rushwa
ambazo anatuhumiwa Hosseh ni Kushindwa kuzibiti ni ununuzi wa Rada
,Kashfa ya Richmond ambapo kamati teule
ya Bunge iligundua kuwepo kwa ufisadi.
Kashfa
nyengine ni ile iliyoibuliwa na Taasisi
ya uchunguzi wa makosa makubwa ya rushwa
(SFO).ilibainiwa kwa baadhi ya vigogo wa Tanzania walipokea rushwa.
Sanjari
hizo pia Hosseah, ameshindwa kuzuia rushwa
katika sakata la Tegeta Esrcow,pia katika kipindi cha miaka 10 alichokaa
madarakani Hosseah anatuhumiwa kufumbia macho uporaji wa mabilioni ya Akaont ya madeni ya nje EPA iliyokuwa Benki kuu (B.O.T)
Pia Kashfa nyengine anayotuhumiwa pia kunyamazi sakata la
Ufisadi wa hati fungani ya Benki Stanbik ambapo kumetokea ufisadi wa zaidi trioni
1.2 za kitanzania
Hakuna maoni
Chapisha Maoni