Zinazobamba

UMESIKIA KUHUSU SARATANI??? HOPSITALI YA OCEAN ROAD YAJA NA HILI,SOMA HAPA KUJ



Watanzania wameshauriwa kuwa na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kwa lengo la kutambua mapema ugonjwa unaowasumbua ili kuweza kupatiwa tiba kwa haraka iwezekanavyo wakiwemo wagonjwa wa Saratani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Diwani Msemo  amesema takwimu zinaonyesha kuwa wagonjwa wengi wa saratani hufika hospitalini wakiwa na hali mbaya ya matibabu.
Amesema tatizo la saratani limekuwa likiongezeka siku hadi siku duniani kote, hasa katika nchi zinazoendelea ikiwemo nchi ya Tanzania  ambapo  kila mwaka wagonjwa wapya wanakuwa takribani 44,000 ambapo kati yao wamekuwa hawafiki hospitalini kupata huduma.
Mkurugenzi huyo wa Saratani amesema asilimia 10 ya wagonjwa kati yao hufika hospitalini katika taasisi ya Oceani Road huku asilimia 80 hufika wakiwa katika hali mbaya yaugonjwa,hali ambayo hupunguza uwezekano wa kutoa matibabu ya kuponyesha ugonjwa huo.
Ameongeza kuwa nchini Tanzania wagonjwa wa Saratani ya Shingo ya kizazi ni wengi zaidi kuliko wagonjwa wa saratani ya matiti  kwa sababu mbinu ya uchunguzi wa saratani ya kizazi ambazo zimekuwa zikitumika kwa miaka 50 iliyopita hapa nchini mbinu hizo hazikupewa kipaumbele kudhibiti saratani hiyo.
Aidha amesema taasisi ya Ocean Road kwa kushirikiana na hoteli ya kunduchi beach wameweza kuwaandaa matembezi ya hisani yenye lengo la kuchangia juhudi za serikali katika kutokomeza saratani ya matiti,kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu saratani ya matiti ,kujua dalili na athari za kuchelewa kupata matibabu.
Kwa Upande wake Meneja Mkuu wa Hotel ya Kunduchi,Paul Garratt amesema matembezi hayo ni miongoni mwa kuwa kumbuka wagonjwa wa saratani kwa hatua nyingine kwa kuwasaidia kuwachangia fedha zitakazoweza kuwasaidia kupatiwa matibabu kwa urahisi zaidi.

Hakuna maoni