CUF YAKINUKISHA TENA,UONGOZI WAIBUKA NA KUILIMA ZEC,YASEMA LIWALO NA LIWE,UCHAGUZI HAURUDIWI,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi wa Chama chacha wananchi CUF,Twaha Taslima akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kupinga uamuzi wa ZEC |
CHAMA cha wananchi CUF kimesema hakipo tayari
kuingia tena kwenye uchaguzi mkuu visiwani
Zanzibar .Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Kauli hii ya CUF inakuja baada ya mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC)bwana Jecha
Salim Jesha kufuta uchaguzi wote na kutangaza kufanyika tena ndani ya siku 90.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi
ya CUF,Twaha Issa Taslima amesema Chama chake hakioni sababu ya kuingia kwenye
uchaguzi kutokana na mwenyekiti wa ZEC kutokuwa na mamlaka ya kikatiba na sheria ya kufuta uchaguzi.
Amesema jambo
linaloshangaza ni kuona mwenyekiti wa ZEC kutangaza kufuta uchaguzi bila ya
kuwashirikisha makamishna wake,
“Hili
linathibitishwa na taarifa ya vyombo vya habari iliyotolewa na makamishna wa
zec kukanusha kuhusika na uamuzi huo wa mwenyekiti wa zec,ambapo hatua hii ni
uvunjwaji wa katiba ya Zanzibar (1984) ibara ya 119(10) inayotaka vikao vya ZEC kuhudhuriwa na
mweyekiti na makamu mwenyekiti na wajumbe wane4 na uaamuzi kuungwa mkono na
walio wengi”amesema Taslima.
Taslima
amesema CUF kwa kimepitia katiba zote
mbili,katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,(1977),katiba ya Zanzibar
ya (1984) sheria ya uchaguzi sura 343 (2010),sheria ya uchaguzi ya Zanzibar
Na.11/1984 na kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge za 2025 na kujiridisha kuwa hakuna kifungu
chochote kinachozipa Mamlaka ZEC ya kufuta uchaguzi uliokwisha Fanyika.
“Kwa
Mantiki hiyo uamuzi uliochukuliwa na mwenyeikiti wa ZEC kufuta uchaguzi wa
Zanzibar na matokeo yake yote ni batili na hauwezi kukubalika”amesema
Hata
hivyo amesema kitendo cha mwenyekiti wa ZEC kutangaza kurejea kwa uchaguzi mkuu
siku (90) tangu tarehe 28/10/2015 alipofuta huu uliomalizika ni kuvunja katiba
kwani katiba ya Zanzibar ibara ya 90 inatamka bayana kuwa mara baada ya
kuvunjwa kwa baraza la wakilishi uchaguzi mkuu utaitishwa ili kuliwezesha
baraza jipya ndani ya siku 90.
“Baraza
la wawakilishi lilivunjwa rasmi tarehe 13/8/2015 na hivyo baraza jipya
linapashwa kukutana si zaidi ya tarehe 13/11/2015.kwa Tangazo la mwenyekiti wa
ZEC,la kurejewa uchaguzi wa siku 90 baadaye,katiba ya Zanzibar itakuwa
imevunjwa jambo ambalo haliwezi kukubalika.
KUHUSU MADAI YA KASORO ZILIZOKUWEPO.
Kuhusu madai
ya kuwepo kasoro kwenye uchaguzi huo zilizotolewa na mwenyekiti wa ZEC,Cuf
wamesema kasoro hizo haziwezi kupeleka uchaguzi kufutwa kwani kasoro za
uchaguzi au malalamiko yoyote ya uchaguzi lazima yawasilishwe kwa fomu maalum
zinazohusika na kuambatanishwa na matokeo na sio kufuta uchaguzi.
Vilevile Chama cha CUF kimewataka waananchi kuwa
watulivu katika kipindi hichi ambapo juhudi kubwa inafanyika.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni