Zinazobamba

CRDB BENK YAJITOSA KWENYE VITA YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU,SOMA HAPO KUJUA


Mkurugenzi wa CRDB Dr.Charles Kimei (katikati) akikabidhi vifaa vya Hospitali kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Musa Nati(kulia) huku Mganga wa Mkuu Manispaa ya Kinondoni Aziz Msuya akishuhudia zoezi hilo
Benki ya CRDB imeikabidhi manispaa ya kinondoni vifaa na dawa zenye thamani ya shilingi milioni kumi na tano kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.
Akikabidhi vifaa vya hospitali na dawa hizo jijini Dar es Salaam kwa mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Musa Noti, Mkurugenzi wa CRDB Charles Kimei amesema wanaimani msaada huo utasaidia kuongeza mapambano dhidi ya kipindupindu kwa kuokoa maisha ya watanzania na kuwataka wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano huo.
IMG_3373
Mkurugenzi wa CRDB Dr. Charles Kimei wapili kushoto akikabidhi vifaa vya hospitali kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Musa Noti.
Pia ameeleza kuwa endapo wataona ugonjwa huo unazidi kuwa tatizo wataendelea kutoa mchango wao ili kuhakikisha maisha ya wateja wao yanakuwa salama wakati wote, halikadhalika maboresho ya huduma za CRDB yanakuja na mfumo mpya utakao wawezesha kufanya kazi kwa ufanisi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Musa Nati amesema kuwa wanaishukuru benki ya CRDB kwa msaada walioutoa kwani kupambana na ugonjwa wa kipindupindu kuna hitaji fedha nyingi ambapo manispaa pekee haiwezi bila kuwa na mchango kutoka kwa wadau mbalimbali.
Vilevile mkurugenzi Nati amewataka watanzania kuzingatia kanuni za usafi ili kuepuka ugonjwa wa Kipindupindu kwa kushirikiana katika masuala ya msingi yenye tija kwa jamii bila itikadi za vyama, dini na kabila.
CRDB imetoa msaada huo ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa mteja yenye lengo la kutangaza huduma bora zitolewazo na benki hiyo.

Hakuna maoni