CHAMA CHA ADC YAWAEKEA NGUMU MAKAPI YA CCM,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti wa Chama cha ADC Mhe. Said Miraj Akisalimiana na mlezi wa chama hicho ambaye sasa ndiye mgombea wa urais zanzibar kwa tiketi ya chama hicho wakisalimiana wakati wa ufumnguzi wa mkutano hu |
CHAMA cha
siasa cha ADC kimesema kamwe hakitampokea mwanachama yeyote kutoka chama
kingine cha kisiasa na kumpatia fursa ya kugombani uongozi,badala yake kimesema
kitampoke na kumpatia nafasi ya kuwa
mwanachama wa kawaida.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Mwenyekiti wa ADC, Said Miraji wakati akifungua mkutano wa mkuu wa chama hicho,ambapo Miraji amesema kwa
sasa kumekuwa na wimbi la wanachama mbali mbali walioshindwa kura kwenye vyama
vyao na kuhamia kwenye vyama vya vingine huku wakipewa nafasi za uongozi kwa
kudai chama chake hakitafanya hivyo kwa kudai wengi hawana nia ya dhati ya
kuwakombo watanzania.
Amesema kuwa sababu ya kuwakataa
wanachama hao wasipate nafasi ya uongozi inatokana na chama ADC kuwepo na
wanachama wenye sifa ya kuongozi kwahiyo haoni haja ya chama hicho kitafute
wagombea nje ya chama hicho.
Aidha,Mwanasiasa huyo machachali ametoa
masikitiko yake kwa Muunganiko wa Umoja wa Vyama vya Upinzani vinavyounda UKAWA kwa kumchukua Waziri mkuu wa
zamani Edward Lowassa na kumpatia nafasi ya kugombani urais,kwa kusema
wamewahadaa watanzania.
Miraji ametaja kuwahadaa huku
Watanzania ni kutakona na Viongozi mbali
mbali wa Vyama hivyo vya Upinzani kumtolea maneno machafu kiongozi huyo pindi
alipokuwa ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Wakati huo huo Chama ADC kinatarajia
kumtangaza mgombea wake wa Urais wa Upande wa Tanzania bara na Zanzibar kesho.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni