BREAKING NEWS.PROFESA LIPUMBA AVAMIWA NA WAZEE WA CUF,MKUTANO WAKE NA WANAHABARI WAOTA MBAWA,SOMA HAPO KUJUA
MWENYEKITI
WA chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba amevamiwa na baraza la wazee
wa Chama hicho, na kumzuia asiongee na waandishi wa Habari.Anaadika KAROLI
VINSENT endelea nayo.
Profesa Lipumba ambaye ni mwenyekiti
mwenza wa Umoja wa vyama vinavyounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA ambaye alitarajiwa kuongea na Vyombo mbalimbali
vya Habari kuhusu mwenendo wa chama hicho leo majira ya saa nne,asubuhi,
Hata
hivyo Waaandishi wa habari walijotokeza makao mkuu ya Chama hicho yaliyopo Buguruni
Jijijini Dar es Salaam Ofsini hapo
wakijazana wananchama wa chama hicho wakiimba nyimbo mbalimbali za chama hicho.
Ilipofikia saa sita kamili huko bado
Profesa lipumba hakujitokeza mbele ya waandishi wa Habari, ndipo waandishi hao
wamkafuata Afisa habari wa CUF ili kutaka kujua kunanini mkutano huo, unachelewa kuanza wakati mda wa
mkutano huo ulitakiwa kufanyika saa nne
asubuhi,
Mara baada ya waandishi hao
kulalamika huko,Ndipo akatokea Naibu Katibu mkuu wa CUF bara Be Magdarena
Sakaya na kusema Kuhairisha Mkutano huo na wanahabari huko akidai profesa
Lipumba amevamiwa na wazee wa chama hicho ndio wamemfanya achelewe kuzungumza
na waandishi wa habari
“Kusema kweli leo Profesa Lipumba
ameshindwa kuongea na waandishi wa habari kutokana na kumvamiwa na
wazee,kwahiyo ikamfanya ashindwe kuzungumza na waandishi wa habari mpaka
amalize kikao na wazee hao na mkutano wenu utaitishwa siku nyengine”amesema Be
Sakaya.
Waandishi wa Habari wakamuliza kiongozi huyo
kwani Profesa lipumba alikuwa anataka kuongee nini kwa waandishi wa habari mpaka wazee hao wakamuzia.
Ndipo akajibu huku akisema hata
yeye afahamu mwenyekiti wake Profesa lipumba alikuwa ataka kuzungumza nini.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni