Zinazobamba

WANAO MTETEA ZITTO KABWE WAJIBU HOJA HIZI,MAANA ANAHUKUMIWA KWA MATENDO YAKE,SOMA HAPA KUJUA

Kiongozi Mkuu wa ACT-Tanzania, Zitto Kabwe akipongezwa na wanachama wake katika mkutano wa mkuu wa chama hicho
Mwandishi ; SAED KUBENEA
      Zitto Kabwe ameanza kuweweseka, anasema kisichopo na kuzingizia wasiohusika
        Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jimboni kwake         anasema hatua ya yeye KUSHUGHULIKIA WEZI KATIKA AKAUNT YA ESCROW, ndiyo chanzo cha kesi yake dhidi ya chadema kutupwa na mahakama.
      Anasema kesi hiyo imetupwa kwasababu amewataja baadhi ya majaji katika wizi huo wa akaunti ya escrow
Alirejea kauli hiyo jumatatu wakati akihojiwa na ITV katika kipindi cha dk 45.
       Hakuna shaka kila aliyemsikiliza Zitto kwa umakini na kufwatilia nyendo zake ndani na nje ya CHADEMA atakuwa amebaini yote aliyoeleza na kukoleza, hayakuwa na ukweli na anapotosha kwasababu ni hizi.
        KWANZA, Safari ya Zitto ya ubunge miaka 10 akiwa chadema imejaa ghiliba, ubinafsi na usaliti. Ndani ya cdm zitto amekuwa akishirikiaana na wanaokivuruga chama, wanaotuhumiwa kutaka kuangamiza maisha ya viongoz wakuu wa chama na wanaotajwa kuwa maadui wa chama.
Katika kipindi chote alichokuwa naibu katibu mkuu wa cdm na mbunge, Zitto hakukisaidia chama kujijenga ata kigoma tu bali aliitumia chadema kujijenga binafsi.
        Kwa mfano uchaguzi wa 2000 cdm ilipata madiwani 5 jimbo la kigoma kaskazin, mwaka 2005 ambapo Zitto aligombea kwa mara ya kwanza chama kilipata madiwani 3 kati ya kata 11. Hii ni kwasababu baada ya kuisha uchaguz wa 2005 Zitto hakufanya tena kazi ya kisiasa jimbon kwake bali alikuwa na kazi ya kukivuruga chadema
Zitto alizunguka nchi nzima kuunda mtandao wa kusaka uenyekiti wa chama na kuwahujum baaz ya wenzake ndan ya chama ili ajinufaishe binafsi.
      Uc haguzi wa 2010 chadema ilizidi kuporomoka kigoma ambako ilikuwa ngome, mkoa ukaangukia kwa NCCR. Jimbon kwa Zitto cdm ikaambulia madiwan 2 kati ya 15.
         Yeye mwenyewe pamoja na kupata msaada mkubwa toka CCM na serikali akajikuta anashinda kwa mbinde.
       Ushindi wake ulipatikana kwa amri ya Yusuph Makamba alekuwa katibu wa CCM. Zitto mwenyewe alishawai kumtaja Jakaya Kikwete kuwa alimsaidia kufanikisha ushindi wake.
       Makamba aliamrisha viongozi na watendaji wa chama chake mkoani kigoma kumuachia ubunge Zitto. Amri hii ilitekelezwa na kumuacha kAma yatima Rodinson Lembo alekuwa mgombea wa CCM.
           Naye Kikwete pamoja na kwenda Kigoma zaidi ya mara 2 kutafuta kura na kunadi wagombea hakuthubutu kutia mguu jimbon kwa Zito.
       Ni matokeo hayo mabovu anayopata toka Kigoma kaskazini yanayomsukuma kuhama jimbo na kukimbilia kugombea Kigoma Mjini anakobadilishana na Peter Serukamba wa CCM nayeenda kugombea kigoma kaskazini
      PILI, Zitto sio mwasisi wa hoja hii ya Escrow kama anavowadanganya watu bali ni Daid Kafulira.
Kafulira aliibua hoja ya escrow mara ya kwanza tarehe 9/5/2014 wakat akichangia bajeti ya waziri mkuu na alitaja had wahusika na kuomba jambo hilo lichunguzwe.
Sio Zitto bali ni Halima Mdee aliyejitokeza kusimama na Kafulira, baada ya Mussa Zungu kumtaka Kafulira afute kauli yake katika kikao cha join cha siku hiyo.
            Kafulira aligoma, William Lukuvi alekuwa waziri wa sera, uratibu na bunge alisimama na kukana tuhuma hizo na kumtaka Kafulira kuzifuta na kuacha kutuhumu watu
Kumbukumbu zinaonyesha ni Halima Mdee alemtaka spika kuunda tume ya kuchunguza jambo hili alisema Kafulira ana ushahid wa kutosha wa jambo hili akahoji “kwann hamtaki athibitishe?. HUYO ALIKUWA HALIMA MDEE NA SIYO ZITTO ZUBERI KABWE
          Mkolezo wa Mdee na king’ang’aniz cha Kafulira ndivyo vilimsukuma Waziri mkuu Pinda kuliahid bunge kulifanyia kaz jambo hili kupitia ofis ya CAG, NA HII NDIVO ILIVOKUWA!!!!
           Hapa ndipo anaingia Spika Anne Makinda, alitoa hadidu za rejea kwa PAC. Ilikuwa kaz rahis soma ripot ya CAG, Chambua vielelezo, andika taarifa na uiwasilishe bungeni. Hiyo ndo ilikua kaz ya “kamat ya Zitto” ilipewa kufanya. BASI HAKUNA JINGINE. Hakuna chochote kipya ambacho kamat hii ilikileta nje ya kile ambacho CAG amekieleza. Hakipo
          TATU, Kunamambo muhimu sana ambayo Zitto hataki kuyaeleza, mojawapo ni hili BILA WABUNGE WA UKAWA KUZUIA MAPENDEKEZO YA KAMATI YAKE, HAKUNA MTUHUMIWA WA ESCROW AMBAYE ANGEWAJIBISHWA.
           Mkakati ulikuwa umeandaliwa na Zitto kwa kushirikiana na wabunge wa CCM na serikali kuzuia watuhumiwa kuwajibika.
         Hili linathibitishwa na Kukwama kwa azimio la kwanza lililomhusu Stephen Masele, naibu waziri nishat na madin ambae alikuwa anatuhumiwa kukaa kimya had mabilion hayo yanachotwa BOT
          Ni hapa ndipo Andrew Chenge mmoja wa watuhumiwa wa Escrow alipopewa fursa ya kupendekeza mfumo wa kuandika maazimio ya bunge; akilenga kuepusha tuhuma nzito zilizoibuliwa na Kafulira na CAG
KAtika hali isiyo ya kawaida, na ilikuwa karibu na usiku wa manane; Zitto kwa sauti ya unyonge na kunyenyekea               ALIRIDHIA MAPENDEKEZO YA CHENGE, yalotaka bunge lisimwagize Rais kuwashughulikia watuhumiwa bali limshauri tu akidai iyo ndo kaz ya bunge-kushauri tu
       Makinda alipomuuliza Zitto iwapo maazimio yote yafwate mkondo huo wa kushauri, Zitto alijibu ANAKUBALI ALICHOSEMA CHENGE na kutamka tena AMECHOKA UBONGO!
           Kama ni kutafuta waliofanikisha hatua za sasa za wanufaika na Escro, Freeman Mbowe hawez kuachwa bila kutajwa’
        Mbowe akiungwa mkono na wabunge wa UKAWA na baaz ya wabunge wa CCM alisema wazi YEYE NA WENZAKE HAWAWEZ KUSHIRIKI KATIKA UAMUZ BATILI JUU YA FEDHA ZA UMMA; Hi indo ilofanya Spika kusimamisha bunge usiku wa manane
      Alicholenga Zitto na wabunge wenge wa CCM kutaka mapendekezo ya kamati yake yasikilizwe na kupitishwa kwa kura yaw eng kilizolewa na hotuba ya Mbowe
        Maazimio yalipokuja kusomwa baadae na Zitto kwa kile kilichoitwa “kupatikana kwa maridhiano” hayakuandikwa na Zitto bali yaliandikwa na wabunge wa UKAWA. Ushaidi upo
         Lakini kama hiyo haitoshi ni Zotto huyuhuyu alietetea kwa nguvu zake zote watuhumiwa wa Kafulira ambao ni Gavana wa Bot, waziri wa fedha, na baaz ya watenaji wa benk kuu kwa kisingizio maofisa wa BOT na serikali waliisaidia kamat yake kupata taarifa muhimu kuhusu wizi huo. Kumbe mwiz akishiriki kukupa taarifa anasamehewa???
        KATIKA MAZINGIRA HAYA, MAJIGAMBO YA ZITTO AMEFUKUZA KAZI WATUHUMIWA WA ESCROW YANATOKEA WAPI???
         Mbona maazimio yake yalizikwa tayari na Mbowe??
Aidha mpaka sasa Zitto hajaeleza juu ya madai ya kumegewa sh million 500 na Sethi. Fedha hizo zilichukuliwa na Zitto kupitia wakili wake, Albert Msando. Zitto amebaki anadai achunguzwe!!!! Nan anayeweza kumchunguza? Marafiki zake?
        NNE, Kama kuna jaji alehusishwa na Escrow si mwingine bali ni jaji John Utamwa. Hukumu zake mbili ndizo za sept 2013 na January 2014 ndizo zilizokuwa zikihusiana na akaunti ya Escrow
      Lakini ni jaji Utamwa huyuhuyu aliyetoa amri ya zuio la Zitto dhidi ya CHADEMA, akitaka Zitto asikilizwe kwanza kabla ya kuhukumiwa. Aliyefuta kesi ya Zitto ni jaji Richard Mziray, na hakutajwa popote ktk orodha ya watuhumiwa wa escrow!!
         Jaji Mziray alihamishiwa mahakama kuu kutoka mahakama ya ardhi na alikabiziwa faili la kes ya Zitto baada ya Jaji Utamwa na majaji wenzake zaid ya 60 kupata uhamisho wa kawaida wa vituo vya kazi
    Zitto akiwa raia huru wan chi hii, ana haki kutoa kauli yake juu ya mambo yanayomhusu na mengne. Lakin kudai kuwa mahakama imesukumwa na feza za escrow kufuta kes yake ni kwenda mbali sana. NI KUTUKANA               MAJAJI NA MAHAKAMA.
Angalia msululu wa watu waloibua na kukomalia wez wa escrow yupo alekuwa CAG, Ludovick Utouh, Kafulira, Mdee, Mbowe, cha kujiuliza kwann watuhumiwa wa escrow waache kuangalia orodha iyo hapo juu na wakimbilie kuwadhuru watetez wao PAC na Zitto walokuwa wanawakinga? HUU NI MZAHA MCHAFU SANA!
          Kwa msingi huu basi, ni muhimu kwa wote wanaomsikiliza Zitto wakarejea hstoria hii ya Escrow, wakarejea ndani ya chama chake, wakarudi nyuma na kuangalia mienendo yake na wakawaangalia wanaomzunguka- wale ambao anawaambia wanachotaka kusikia.
            Wakifanya ivo watagundua huyu bwana si mtetezi wa maslai ya taifa kama anavojitambulisha. Huyu amekuwa akijitetea binafsi, amekuwa akisaliti harakati za mabadiliko na amekuwa wakala wa maofisa wa usalama wa taifa mwaka wa 7 sasa

4 comments

Ndimbo Furniture said...
This comment has been removed by the author.
Ndimbo Furniture said...

Duuuuh....kwahyo zito n mzgo Wa ""chukua chako mapema"""

Anonymous said...

Wewe Kubenea huna jipya bali unalipwa na Mbowe kumchafua Zitto kwani wewe hujawahi kujibu baadae kujua umejibu hata hujui ulichojibu, halafu hujui kuwa mtu akifanya malekebisho ya mtu mara nyingi hujikita kwenye maazimio hayo hayo bali huyaboresha tu.
Ningeweza kujibu hoja moja moja lakini nitakuwa Najibu mtu ambae katumwa hata hawezi kuelewa maana umezibwa masikio @KUBENEA

Anonymous said...

Na wewe ni walewale tangaza wazi tujue na wewe ni