KUBWA-AZAM MEDIA YAIBOMOA BBC YAMCHUKUA KIFAA WAKE MUHIMU,WAAPA KUZOA WENGI SOMA HAPA KUJUA
![]() |
| Wafanyakazi wa Shirika la Utangaza la uingereza BBC wakimuaga na kumpatia jezi ya Mpira Charles Hillary juzi nchini Uingereza |
MTANGAZAJI maarufu wa Shirika la
Utangazaji la uingereza (BBC) Charles Hillary
hatimaye ameacha kazi kwenye shirika hilo na kujiunga rasmi na Azam Media.Anaandika
KAROLI VINSENT endelea nayo
Charles Hillary ambaye
amejipatia umaarufu mkubwa barani Afrika
na maeneo mbalimbali duniani kwa ustadi wake wa kutangaza mechi za mpira wa
miguu yaani soka kwenye maeneo mbalimbali hususani ligi za ulaya na Afrika ambapo sasa amejiunga
na Azam media na kupewa mkataba mnono.
Kwa mujibu wa mtoa
taarifa wetu aliyoko kwenye Kampuni ya Azam Media ambayo inamilikiwa na
Mfanyabishara mkubwa hapa nchini bwana Said Salim Bakhresa zinasema mtangazaji huyo
atachukua nafasi ya Tido Muhando katika kuendesha kampuni hiyo ambapo sasa Tido
muhando atakuwa chini yake.
Azam
Media ambayo hivi karibuni wamefungua studio za kisasa kabisa zilizoko Tabata
Relini Jijini Dar es Salaam ambazo zimegharimu zaidi ya Bilioni 54 pesa za kitanzania,Taarifa zainadai kitendo cha
Mfanyabiashara huyo kumleta Charles Hillary ni kutaka kuboresha maudhui ya
vipindi vya runinga hiyo viendane na ubora wa Studio zake zilizopo sasa.
Charles Hillary ambaye juzi teyari alikuwa ameshawaaga wafanyakazi
wenzake waliokuwa wanafanya kazi pamoja huko BBC na kuwahakikisha kujiunga na
Azam media.
.jpg)
.jpg)
No comments
Post a Comment