Zinazobamba

JIJI LA DAR KUZIZIMA LEO,NI TAMASHA KUBWA LA PASAKA KUPAMBA MOTO,SOMA HAPA


 Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayetambulika kwa jina la Rebecca Malope akipungia  mkono mashabiki wake hawapo pichani mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA) jioni hii tayari kwa kutumbuiza katika tamasha la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka linalofanyika kesho kwenye uwanja wa michezo wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo Solly Mahlangu mwanamuziki nguli mwingine wa muziki wa injili kutoka nchini humo atawasili kesho na kujiunga moja kwa moja na tamasha hilo.Kulia ni Alex Msama Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion.
Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayetambulika kwa jina la Rebecca Malope akivishwa skafu ya bendera ya Taifa ya Tanzania na mmoja wa maofisa wa kampuni ya Msama Promotion Bi Nyakwesi.

 Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Rebecca Malope akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  usiku huu tayari kwa kutumbuiza kesho kwenye tamasha pa Pasaka.Kuklia kwake ni Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd,Bwana.Alex Msama akitabasamu.

No comments