HOT NEWS.UKAWA WAMEANZA MDOGOMDOGO KUELEKEA OCTOBA,NCCR WATOA KIFAA CHAO SOMA HAPA KUJUA
| Faustin Sungura (katikati), Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi NCCR – Mageuzi akimkabidhi fomu ya kugombea urais mwakilishi wa Dk. George Kahangwa, Mawazo Athanas (kushoto) ambaye ni Katibu Mkuu Vijana Taifa wa chama hicho. |
CHAMA cha NCCR-Mageuzi,
kimemkabidhi, Dk. George Kahangwa, Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa chama
hicho, fomu ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka
huu.Anaandika Pendo Omary… (endelea).
Fomu hiyo ambayo imelipiwa Sh. milioni
moja na imekabidhiwa na Faustin Sungura- Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi
ya chama hicho huku Dk. Kahangwa akiwakilishwa na Mawazo Athanas, Katibu Mkuu
Vijana Taifa.
Machi
mwaka huu, Mwenyekiti wa Kitengo cha vijana wa NCCR- Mageuzi, Deo Meck,
aliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho, kuwa Kahagwa,
ndiye aliyependekezwa na vijana kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais.
Akizungumza kabla ya kukabidhi fomu
hiyo, Sungura amesema “leo chama kinafungua rasmi pazia la wagombea ndani ya
chama kwa kukabidhi fomu ya urais kwa ndugu George Lenarld Kahangwa”.
“Kahangwa ni mtoto wa saba katika
familia ya mwalimu Gabriel Kahangwa na Anastazia Kakunyeta. Ni baba wa familia
ya mke mmoja na watoto wawili. Ni mwanachama aliyelelewa katika maadili na
itikadi ya chama chetu,” amesema.
Sungura amesema Kahagwa alizaliwa 5 Mai
1969 na chama hicho hakina mashaka yoyote na uwezo wake wa kuwatumikia
watanzania kwa nafasi nyeti.
“Pamoja na pazia la wagombea urais
ndani ya chama kufunguliwa rasmi, chama kinawaomba watanzania kujiandaa
kisaikolojia kupokea mgombea urais wa Tanzania Bara au Zanzibar ama Waziri Mkuu
kupitia Ukawa,” amesema Sungura.
Ukawa ni Umoja wa Katiba ya Wananchi,
unaovishirikisha vyama vya Chadema, NCCR- Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF) na
National League Democrat (NLD).
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu
hiyo kwa niaba ya Dk.Kahagwa, Athanas amesema “Machi tuliitisha mkutano na
waandishi wa habari. Tulieleza kuhusu kumuomba kugombea urais kupitia chama
hiki. Baada ya kumuona alitukubalia rasmi. Tumechanga fedha na leo
tumemchukulia fomu.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi
ndani ya chama hicho, 1 Aprili hadi 15 Juni mwaka huu, ni kipindi cha kuchukua
na kurejesha fomu za wagombea urais.
Aidha, 30 Aprili hadi
15 Juni, ni kuchukua na kurejesha fomu za wagombea wa udiwani. 15 Juni hadi 20
Julai, watachukua na kurejesha fomu wagombea uwakilishi/ubunge.
Kumbukumbu za chama hicho zinaonesha
mwaka 1995, Augustin Mrema ndiye aliyekuwa mgombea urais akifuatiwa na marehemu
Dk. Sengondo Mvungi mwaka 2005 na Hashim Rungwe mwaka 2010.
Chanzo ni
Gazeti la Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment