HABARI KUWA,SAMWEL SITTA ACHARUKA,AWASIMAMISHA VIGOGO TRL,WAMEITIA HASARA BILION 230 SERIKALI,SOMA HAPA KUJUA

WAZIRI wa
Uchukuzi Samwel Sitta (pichani) amewasimamisha Kazi Vigogo wa Juu wa Mamlaka ya Reli ya kati nchini TRL kutokana na kuitia hasara
Serikali inayofikia Bilioni 230 kwenye ununuzi wa mabehewa ambayo yamebainika
ni ‘Feki’Anaripoti KAROLI VINSENT endelea nayo.
Watendaji hao waliosimamishwa kazi ni
Mkurugenzi Mtendaji Kipallo Kisamfu,Mhandisi mkuu wa mitambo Ngosowile
Ngosomiles,Mhasibu Mkuu Mbaraka Mchopa,
Wengine ni Mkaguzi mkuu wa ndani wa
Kampuni Jasper Kisiraga,pamoja Meneja Mkuu wa Manunuzi Fedinard Soka.
Akitangaza uamuzi huo mda huu Jijini
Dar es Salaam Waziri wa Uchukuzi Samweli Sitta wakati wa mkutano na waandishi
wa habari ambapo amesema baada ya kupokea ripoti ya Tume iliyoundwa na waziri
aliyekuwepo kwenye wizara hiyo Harrison mwakyembe na kumkabidhi ripori
imeonyesha mabehewa hayo ni mabovu hayafai kutumika kupakia Abiria.
“Baada ya kupata Ripoti hii
tumejidhilizisha wazi kwamba mabehewa haya ni mabovu na hayafai kutumika kabisa
tena mengi yanakasoro kubwa na hayawezi kutembea kabisa na nilipogundua mabehewa
haya ni mabovu nikayazuia ”Amesema Waziri
Waziri Sitta ameongeza kuwa licha ya
kuzuia uigizaji wa mabehewa hayo jambo ambalo
anadai limemshangaza ni kitendo cha watendaji hao kutoa kutoa pesa zote
kwenye kampuni inayotengeneza mabehewa hayo kinyume na taratibu za umma.
“Yaani waandishi wa Habari nimeshangaza
sana na hujuma ambayo inafanywa na watendaji hawa wa Reli ambayo sitegemea
kabisa na siwezi kufumbia macho maana unapoipa tenda kampuni itengeneza na
Mabehewa na kuyaleta inatakiwa utoe pesa kwa mafungu,yaani hatua ya kwanza
unatoa asilimia 40 ya fedha”
“Kabla ya hatua ya pili unatoa fedha baada ya
kuyapokea mabehewa nusu na hatu ya pili sasa unatoa asilimia 40 tena mabehewa
yanakuwa yemekuja yote na asilimia 20 inatoa baada ya kuyajalibu mabehewa
yanafika yanatembea vizuri hadi kigoma au la,sasa jambo la kushangaza watendaji hawa hawajafuata
kanuni hizo wametoa pesa zote Bilioni 230,wakati ni tofauti kabisa na sheria za
Serikali”ameongeza Waziri Sitta
Aidha, Waziri Sitta amesema baada ya
kubaini hali hiyo ndipo amechukua hatua ya kusimamisha watendaji hao kupisha
tume ya uchunguzi iwachunguze kutokana kuvunja kununi kwa kutoa fedha zote.
“Baada ya kubaini hawa watendaji
wamefanya uzembe huu nimewasimamisha kazi,ili kupisha uchunguzi wa
kamati,ambayo inayoundwa na kukushirikiana Ofisi ya kupambana na rushwa (TAKUKURU),Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu,Mamlaka ununuzi katika sekta ya Umma (PPRA),wizara ya
Uchukuzi pamoja na ofisi ya mkaguzi mkuu wa Hesabu ya Serikali (CAG) na nimeipa
wiki tatu iwe imekamilika kuchunguza Uzembe huu”amesema Waziri Sitta.
Vilevile
Waziri Sitta amesema kwa sasa ameitaka Bodi ya Wakurugenzi Kampuni ya Reli ikae
kikao cha Dharura kwaanzia kesho na kuteua watendaji wengine kuziba nafasi
zao.
Katika
hatua nyingine Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta amemuondoa kabisa katika nafasi
aliyokuwa amesemamisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Bwana Madeni Kipande
baada ya Tume aliyoinda kumaliza kazi yake.
Waziri Sitta amesema kwa mujibu wa Ripoti ya tume hiyo imebaini mkurugenzi huyo kushindwa
kabisa kuisimamia Bandari hiyo na kusababisha matatizo kwa wateja.
“Baada kuisoma taarifa ya tume na
hatimaye kushauriana na taasisi mbali mbali zinazohusika na masuala
haya,tumeridhika pasipo mashaka ndugu kipande afai kuongoza mamlaka hii ya
bandari kutokana na kutokuwa na sifa tena amesababisha matatizo”
Amebainisha kuwa kwa sasa nafasi hiyo
itaendelea kushikwa na Awadh Massawe,na huku bwana kipande akirudishwa Wizarani
hapo kutafutiwa kazi nyingine.
No comments
Post a Comment