HABARI KUBWA LEO-UFISADI WA BILION 230 ZA MABEHEWA 'FEKI'MAZITO YAIBUKA SASA WAZIRI MWAKYEMBE KITANZINI,KAFULILA NAYE ARUSHA KOMBORA,SOMA KUJUA
| pichani ni Katibu mkuu Wizara ya Uchukuzi Shaaban Mwinjaka, akiyabokea miongoni mwa mabehewa 200 ambayo ni mabovu na Fullhabari.blogs ulishuhudia kipindi yanaingia nchini |
ALIYEKUWA Waziri wa Uchukuzi ambaye sasa ni waziri wa ushirikiano
wa Afrika Mashariki Dokta Harrison Mwakyembe amehusika kwa kiasi kikubwa kwenye Kashfa ya mabehewa Mabovu ya mizigo 274, iliyoitia hasara Serikali ya Kikwete zaidi ya Bilioni
230 ,(Mtandao huu Umeelezwa).Aaandika KAROLI VINSENT,endelea nayo.
“Waziri Mwakyembe ambaye alijivika vazi
la kondoo kwa umma kana kwamba ni miongoni
mwa mawaziri wanaofanyaka kazi kwa weledi kwa kuweza kulinda mali za umma,ni
wazi vazi hilo limeanza kumvuka.”
Taarifa za Dokta Mwakyembe kuhusika
kwenye Ufisadi huo mkubwa kabisa kwenye masuala ya Reli nchini kuwai tokea tangu Uhuru inakuja ikiwa
siku moja kupita baada ya waziri wa
Uchukuzi Samwel Sitta kuwasimamisha watendaji wa Juu wa Mamlaka ya Reli ya Kati
nchini TRL kutokana na kashfa hizo, ili kupisha uchunguzi juu ya tuhuma hizo.
Tume hiyo ya uchunguzi ambayo inafanywa kwa kushirikiana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi katika Sekta ya Umma (PPRA), na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,ambayo itachukua wiki tatu kuchunguza tuhuma hizo
Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wetu
aliyoko kwenye wizara ya Uchukuzi ameuambia mtandao huu kwamba ni wazi
serikali inafanya kiini macho kuwasimamishwa Watendaji hao na anadai ni kama
inafanya kitendo cha kuwatoa kafara ili kuwalinda mawaziri waliohusika kwenye
ufisadi huo.
“Hapo ni anachofanya sitta ni kiini macho
tu,aiingii akilini kabisa yaani watendaji hao wadogo wa TRL,waamue na wafikie
makubaliano ya kuiilipa kampuni ya India
Bilioni 230 zote bila kupata Baraka za waziri wa Uchukuzi na hata Waziri wa
Fedha?maana pesa nyingi sana hizo Bilioni 230 ndugu sio pesa ndogo hapo kuna
msululu wa Mawaziri wengi kuhusika,na anachofanya Sitta ni kudanganya umma tu”
Waziri Sitta aliwasimamisha watendaji hao
kwa kile anachodai kuvunja makubaliano ya Mkataba kwa kitendo cha kuilipa Kampuni ya Hindustan & Industrial
Engineering Limited ya India asilimia 1oo za pesa kabla ya kumaliza mkataba,
Kwa mujibu wa Waziri Sitta anasema pesa ziingetakiwa zilipwe kwa mafungu yaani
asilimia 50 za kugiza na asilimia 50 iliyobaki ingelipwa pale mabehewa hayo
zaidi ya 200 kuwasili na kuyajalibu kama
yanafaa au la.
Watendaji wa TRL waliosimamishwa na Waziri Sitta
ili kupisha uchunguzi ni Mkurugenzi
Mtendaji, Kipallo Kisamfu, Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosomwile Ngosomiles,
Mhasibu Mkuu, Mbaraka Mchopa, Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Jasper Kisiraga na Meneja
Mkuu wa Manunuzi wa kampuni hiyo, Ferdinand Soka.
Chanzo kingine kinasema kitendo cha Rais Kikwete kumtoa
waziri Mwakyembe wizara ya uchukuzi kunatokana na kujilidhisha pasipo na shaka
waziri huyo alihusika na kuleta mabehewa hayo mabovu.
“Sikufichi Yule bwana,
Kikwete kamuokoa sana maana alijua kwa umakini wa vyama vya upinzani
wasingekubali na wangelipeleka suala lile Bungeni na yangefichuka mengi sana maana
ufisadi ni mkubwa sana na amgusi waziri huyo wako wengi sana,wewe unafikili
hata huyo Mwigulu angepona naye? naye angeisha tu pesa hazitoki bila wizara ya
fedha kulidhia”
Kwa upande wake naye Mbunge wa Kigoma
kusini David Kafulila ameumbia mtandao huu kwamba Malipo ya Bilioni 23o kwenye
kampuni hiyo ya India hayawezi kutolewa bila idhini ya kikao cha baraza la
mawazili na anadai kama ingekuwa nchi makini hapa kungetakiwa hata waziri
mwakyembe pamoja na katibu Mkuu Wizara yaUchukuzi wangefukuzwa kazi na
kufikishwa mahakamani.
“Bilioni 230 zinapotea hivyo sio pesa
ndogo haiwezekani watendaji hao wandogo waidhinishe pesa hiyo bila waziri Mwakyembe
kujua na hata Katibu mkuu uchukuzi bila kujua kama kungekuwa na serikali makini sana hata wasingebaki hata kidogo,sema
tumazoea kulindana lindana tunaacha
lipite”amesema Kafulila
| Mabehewa yao mabovu yakiwa bandarini |
Kafulila ameongeza kuwa Kanuni na taratibu chini ya
Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2004 (ambayo ilifutwa na Sheria Namba 7 ya
mwaka 2011) zilikiukwa.
“PPRA imebaini kuwa TRL
waliingia mkataba na kampuni ya Hindusthan Engineering and Industries Limited
ya India bila kujiridhisha kuhusu uwezo wa kampuni hiyo kama ilivyoelekezwa
kwenye nyaraka za zabuni,” amesema Kafulila.
Hivyo,amesema TRL
ilikiuka kifungu cha 53 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma na matakwa ya nyaraka za
zabuni ambazo zilitaka uchunguzi huo ufanyike.
No comments
Post a Comment