DC MAKONDA ACHARUKA ,AUNDA TUME KUCHUNGUZA MADUDU KINONDONI,SOMA HAPA KUJUA
MKUU wa
wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (pichani)ameunda tume ya watu wa tano kuchunguza
malalamiko ya Wananchi juu ya Ubovu wa barabara na miundombinu mingine ambazo
zinadaiwa kujengwa chini ya kiwango.Anaandika KAROLI VINSENT,Endelea nayo.
Hayo yamesemwa na Makonda leo Jijini
Dar es Salaam wakati na mkutano na Vyombo vya Habari ambapo amesema tangu
akabidhiwe nafasi hiyo amekuwa akipata malalamiko mbalimbali kutoka kwa wakazi
wa wilaya ya Kinondoni juu ya Ubovu wa barabara ambapo Wakazi hao walikuwa
wakisema barabara hizo zinajengwa chini ya kiwango.
“Yaani wananchi wanasema barabara
zinaubovu mkubwa,kwa kiasi Lami inawekwa leo lakini haimalizi miezi Sita
inabanduka na inaacha mashimo,Mitaro inachimbwa mifupi kuliko mahitaji
halisi,barabara zinakuwa nyembamba kutoka kushoto kwenda kulia,yaani wananchi
wanaona kwamba hakuna serikali ya kuona hali hii”amesema Makonda.
Makonda ameongeza kuwa baada ya kupata
malalamiko hayo,yeye kama kiongozi wa serikali amesema haoni haja ya kuacha
uzembe huo,na ndio maana ameamua kuunda tume ya watu mbalimbali wa masuala ya
ujenzi kuchunguza malalamiko hayo ndani ya siku 21 na akabidhiwe ripoti kamili.
Aidha,Makonda aliwataja watu katika
tume hiyo ni Enginia Julius Mamilo ambaye atakuwa mwenyekiti wa Tume
hiyo,Enginia Ronald Rwakatare naye pia atakuwa Katibu.
Mbali ya Viongozi hao watume DC Mkonda aliwataja wajumbe wa Tume hiyo ni John
Malisa,Abednego Lyaga pamoja na Enginia Patrick Balozi.
Kwa mujibu wa Makonda anasema pindi
atakabidhiwa ripoti huyo atachukua hatua kali ikiwemo kuwafukuza kazi watendaji
waliohusika na uzembe huo.
No comments
Post a Comment