Zinazobamba

KUBWA-MCHUNGAJI MSIGWA ARUSHIA KOMBORA SERIKALI YA KIKWETE,SOMA HAPA KUJUA


NA KAROLI VINSENT
       MBUNGE wa Iringa Mijini (CHADEMA) Mchungaji Piter Msigwa ni kama ameishukia serikali ya Chama cha mapinduzi CCM inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete na kusema ni Serikali hatari ambayo haitakiwi kupewa nafasi tena, kutokana kuzidisha anaodai ni utendaji mbovu na kuwaacha wananchi wakilalamika na maisha magumu.
          Vilevile Mchungaji Msigwa amesema pia Rais Kikwete asiwakemee viongozi wa dini pindi wanapoikataa Katiba iliyopendezekwa na Bunge Maalum la Katiba kutokana na katiba hiyo kujaa ghiliba nyingi pamoja na ubabe kwenye upitishaji wake ambapo anadai kiongozi wa kweli wa dini hawezi kuruhusu hali hiyo.
          Kauli ya Mchungaji Msigwa ameitoa leo wakati alipokuwa anahojiwa na kituo cha Redio cha Magic FM katika kipindi cha Morning Magic ambapo amesema kwa sasa Taifa limekosa dira kutokana na Viongozi waliopo madarakani kuzidisha undugu yaani anadai  ndio unaochangia watanzania kuwa masikini wa kutupwa.
             Mchungaji Msigwa ambae ni Waziri Kuvuli wa Maliasili na Utalii amendelea kusema hata hali ya sasa ya Viongozi wa dini kutoa matamko mazito kuhusu mambo mbalimbali ya nchi ni ishara ya wazi tayari viongozi hao wameshaichoka Serikali iliyoko madarakani.
          “Nani asiyejua kwamba mwanzoni viongozi hawa dini walikuwa upande wa Serikali ya CCM,lakini leo wameona wazi kwamba Serikali hii haina tija na imejaa uhasama ndio maana wao wameamua kuwahasa waumini hao kuyakataa mambo mabaya na kiongozi wa dini lazima afanye hivyo”ameongeza Mchungaji Msigwa.
            Aidha, Mchungaji Msigwa amesema kuwa kitendo cha Rais Jakaya kikwete kuwatupia lawama viongozi wa dini kwa vitendo vyao vya kuwafosi waumini wao kuikaa Katiba pendendekezwa,ni kutaka huruma kwa viongozi wakiroho.
        “Namshanga sana anavyosema  viongozi wa dini kuwafosi waumini wao kuikataa katiba hiyo,wakati yeye mwenyewe amesahau kwamba alitumia idara zake mbalimbali za Serikali ikiwemo TBC kuwataka wananchi waipigie ya ndio lakini hilo halikuona lakini leo analiona la viongozi wa dini,ukweli katiba ile ni mbovu”amesema
  


No comments