Zinazobamba

BREAKING NEWS-NAULI ZA MABASI ZASHUKA,WAGOMA KUSHUSHA MENGINE KISA USUMBUFU WA CHENJI,SOMA HAPA KUJUA


MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa nchi Kavu na Majini nchini (SUMATRA) imeshusha Nauli kwa kiwango kidogo kwa wasafiri kwa Masafa marefu yaani kutoka mkoa moja hadi mkoa mwengine kwa  asilimia 7.8.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
    Vilevile Mamlaka hiyo imegoma kushusha nauli za ndani ya mikoa husika, baada ya kubaini kiwango kilichoshushwa cha Shilingi 25 toka kwa nauli iliyopo sasa ambayo wanadai italeta usumbufu kwa Abaria na Wamiliki wa Mabasi.
         Hayo yamesemwa Mda huu Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mkuu wa (SUMATRA) Gilliard Ngewe wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema hatua hiyo imetokana na maamuzi ya Bodi ya Sumatra kufanikisha zoezi la ukokotoaji ambao anasema ukotoaji huo uliangalia mambo mawili ya msingi yaliyosemwa na wadau wa Usafilishaji.
   Mambo hayo ni Kushuka kwa Mafuta kwenye masoko mbalimbali na kushuka kwa kodi ya Uingizaji wa Magari mapya ya Usafilishaji nchini.

“Baada ya kuangalia vigezo hivyo baraza ililifikia hatua ya kushusha nauli za mabasi ya ndani yanayofanya shughuli zake katika mkoa husika kwa shilingi 25,ila baada ya kushauliana tukaoni kushusha kwa kiasi hicho kitaleta usumbufu na kwa wateja,na tukafikia  uamuazi wa kuacha nauli za mwanzo itumike’

"Nahapa tumeshusha nauli za mabasi ya masafa marefu tena yakutoka mkoa mmoja kweda sehemu nyingine  ,”amesema Ngewe   
          Aidha,Amesema kulingana na ukokotoaji wa Nauli hizo Mamlaka hiyo imezingatia Kanuni za huduma za Abiria zinazoainisha Aina nne ya Madaraja ya Mabasi.

         Hata hivyo amesema kuwa viwango hivyo vipya vitaanza kutimika kwaanzia rasmi tarehe 30 Aprili mwaka huu,na akawata wamiliki wa Mabasi pamoja na Wafanyakazi wake kutoza Viwango vya Nauli vilivyotolewa na Mamlaka usika.


Viwango vya Nauli kutokana na Ukotoaji vya Mabasi ya ndani ya mkoa usika ambapo ukokotoaji wa viwango vipya,Sumatra imeacha nauli zinazochajiwa kwa sasa kama unavyoona hapo, zitumike kutokana na viwango vipya vya nauli iliyokotolewa ya pungufu la shiringi 25
ingeleta usumbufu kwa Abiria,soma hapo,

Njia

Nauli ya sasa
Nauli iliyokokotolewa
0-10
            400
           
376.77 

       11-15KM          
    450

448.62
             16-20km
        
           500
          
465.34 
            21-25km
        
600           

583.34 
26-30 km
         750
742.74 
   Viwango Vipya vya Nauli za Mabasi ya masafa marefu yaani kutoka mkoa mmoja hadi mwengine zimeshuka kama unavoona kwenye jedwali lifuatalo zimepungua
Daraja la basi

Nauli ya sasa
TZS /Abiria km
Viwango vipya vya nauli vilivyoridhiwa
Daraja la kwanza la chini
(Low ordinary -lami
            36.89
           
34.00
       Daraja la kawaida chini
Lower ordinary  Bus         
   46.11

42.50
             Darala la kawaida la juu
Upper ordinary Buss
        
          
           -
44.96
          Daraja la kati
Semi-luxurry Buss
        
53.22           
44.96

No comments