BENKI YA NMB YAZIDI WAJALI WATEJA WAKE,YAZINDUA KITU KIPYA,BWANA KIVARIA ASEMA NI HUDUMA POA SOMA HAPA KUJUA
| Pichani ni Mkuu wa Kitego cha Huduma Mbadala wa Benki ya NMB Bwana George Kivaria Akifafanua Jambo, picha na Maktaba |
KATIKA
kuonesha inawajali wateja wake nchini Beki ya NMB imezindua Huduma yake bora ya
kutoa pesa kwa haraka inayojulikana kama(NMB CHAP CHAP)Anaandika KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Akitambulisha Huduma hiyo leo Jijini Dar es
Salaam Mkuu wa Kitengo cha Huduma Mbadala wa Benki ya NMB nchini Bwana George
Kivaria wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari ambapo amesema Huduma ya hiyo
wameianzisha mahususi kwa ajili ya kuwasogezea wateja wa Benki hiyo karibu na
makazi yao ili iwape urahisi katika kutoa pesa.
“NMB Chap chap ni akaunti kama akaunti
nyingine isipukuwa inafunguliwa kama teknohama ya vifaa maalum kama simu na pos
nje ya matawi yetu kwenye maeneo ya
wateja,vilevile inafunguliwa kwa mashart nafuu.”
Bwana Kiviria ameongeza kuwa Huduma ya Benki
chap chap itawasaidia wateja walioko mbali na Benki ya NMB ili wapate akaunti
zakibenki na hatimaye waingie wote kwenye mfumo wa wigo rasmi wa kifedha ambapo
anasema kwa kufanya hivyo anadai watajihakikishia ukuaji kwenye biashara kwenye
Benki hiyo.
Sanjari na Faida hizo Bwana Kirivia
alizitaja taratibu za ufunguaji wa Akaunti katika Benki hiyo ni Mteja kuja pesa
ya ths 100,00/yaani Tsh 5500/=garama za Kadi n ash 4500/=nyingine kama amana ya
Akiba.
Aidha, Bwana Kivira aliwataka wateja wa
Benki NMB wakitaka kufungua Akauni za Chap chap wajitokeze na Pasipoti ya
kusafiria,kadi ya kupiga kura,kadi ya kulipwa pension,utambulisho toka Afisa
Mtendaji wa Kijiji,Leseni ya Udereva na kitambulisho cha Taifa..
Pamoja na hayo amebainisha kuwa wateja
wa Benki hiyo watanufaika kwa kuingia kwenye mfumo anao dai ni mzuri wa
kibenki,kupata riba na kufaidi gharama
nafuu za kibenki pamoja na kutunza Fedha pahala salama na madhubuti.
No comments
Post a Comment