UFISADI WA KUTISHA TRL-KAFULILA ARUSHA BOMU ZITO KAMA KWENYE ESCROW SOMA HAPA KUJUA
DAVID Kafulila-Mbunge wa Kigoma Kusini
(NCCR-Mageuzi) ameweka hadharani udhaifu ulioainiswa na Mamlaka ya Udhibiti wa
Ununuzi wa Umma (PPRA), katika michakato ya zabuni mbili za manunuzi ya
mabehewa. Anaandika Pendo Omary …
(endelea).
Zabuni hizo ni
namba PA/113/2012-13/ME/G/OE/013 ya ununuzi wa mabehewa 25 ya
mizigo (supply of New Ballast Hopper Bogie Wagons).
Zabuni ya pili
ni namba PA/113/2012-13/ME/G/OE/014 ya ununuzi wa mabehewa ya mizigo 274
(supply 274 New Goods Wagons).
Kafulila
ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Viwanda na Biashara, ndiye muasisi wa
kashfa ya ufisadi wa sh. 306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow
ambao umeng’oa mawaziri wawili na Mwanasheria Mkuu.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, amesema taarifa ya awali
iliyotolewa Machi mwaka huu na PPRA kuhusu uchunguzi wa mchakato wa ununuzi wa
mabehewa uliofanywa na Shirika la Reli Tanzania (TRL), umebaini upungufu
ufuatao;
Kanuni na taratibu
chini ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2004 (ambayo ilifutwa na Sheria
Namba 7 ya mwaka 2011) zilizotumika katika ununuzi huo.
“PPRA imebaini kuwa TRL waliingia mkataba na kampuni ya Hindusthan
Engineering and Industries Limited ya India bila kujiridhisha kuhusu uwezo wa
kampuni hiyo kama ilivyoelekezwa kwenye nyaraka za zabuni,” amesema Kafulila.
Hivyo, TRL ilikiuka
kifungu cha 53 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma na matakwa ya nyaraka za zabuni
ambazo zilitaka uchunguzi huo ufanyike.
Aidha, uchunguzi umebaini kuwa zabuni
hizi zilitangazwa kwenye magazeti ya ndani peke yake bila kutangazwa kwenye
gazeti moja la kimataifa kama inavyoelekezwa kwenye nyongeza ya kwanza ya
Sheria ya Ununuzi wa Umma.
“Hii inapunguza ushiriki wa kampuni za nje kwa kutopata taarifa ya
tangazo la zabuni hiyo,” inasomeka sehemu ya taarifa ya PPRA.
Aidha, uchugunguzi
umebainisha pia kuwa uandaaji wa mahitaji (specifications), uliofanywa na Idara
Hitaji kuhusu mabehewa yaliyokuwa yanahitajika ulikuwa dhaifu.
Hii imedhihirika
kutokana na kamati nne za ukaguzi kutumwa India kwa nyakati tofauti kukagua
utengenezaji wa mabehewa hayo na kuendelea kutolewa mapendekezo ya marekebisho
ya mahitaji ya mabehewa hayo.
Taarifa hiyo
inasomeka “utekelezaji wa mikataba yote miwili TRL walichelewa kutekeleza
maombi ya malipo ya awali na iliathiri muda wa utekelezaji wa mikataba hiyo”.
Pia, PPRA imebaini
menejimenti ya TRL haikuwa makini kushughulikia maombi ya kuongezewa muda
yaliyokuwa yanawasilishwa na kampuni ya Hindusthan Engineering Limited.
Kwa mfano; katika
mkataba wa zabuni PA/133/2012-13/ME/G/OE/014, kampuni hiyo iliwasilisha maombi
13 Mai, 2014 ya kuomba kuongezewa muda wa mkataba hadi 14 Disemba, 2014.
Maombi hayo
yaliidhinishwa na TRL 16 Mai, 2014 na muda wa mkataba uliongezwa hadi 30
Septemba 2014.
“Kwa hali ya nchi yetu ilipofika ni lazima hii taarifa itoke, watu
wajue kinachoendelea. Hivyo kwa taarifa ya awali ya PPRA ni lazima hatua
zichukuliwe na mamlaka husika,” ameongeza Kafulila.
Mkataba huo
ulisainiwa kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) na kampuni ya Hindusthan
Engineering and Industries ya India 21 Machi 2013, wenye thamani ya Dola za
Kimarekani 2,561,187.50.
Zabuni hii
iligawanyika katika makundi matatu: kundi la kwanza mabehewa ya mizigo 174
(Covered Large Bogie Wagons), kundi la pili mabehewa 50 (Petro Tank Bogie
Wagons) na kundi la tatu mabehewa 50 (Container Carrier Wagons).
Mkataba wa ununuzi
wa mabehewa 274 ulisainiwa kati ya TRL na kampuni ya Hindusthan Enginneering
and Industries Limited ya india kwa thamani ya jumala ya Dola za Kimarekani
28,487,500.
PPRA inafanya uchunguzi huo kwa kuangalia iwapo taratibu za
manunuzi zilizoainishwa katika Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma
zilizingatiwa; utekelezaji wa mkataba ulizingatia masharti na taratibu
zilizoaninishwa kwenye mkataba;
Ilichunguza
iwapo mabehewa yaliyopokelewa ni mapya au yametumika na itatoa mapendekezo ya
kuboresha utendaji kazi wa TRL au hatua za kuchukua dhidi ya watakaobainika
kuhusika katika ukiukwaji wa Sheria, kanuni na Miongozo ya Manunuzi ya Umma.
Chanzo ni
Mwanahalisi.online
No comments
Post a Comment