Zinazobamba

NEC YAENDELEZA KIBURI CHAKE,SASA WAUNGANA NA PINDA KUFOSI KURA YA MAONI.SOMA HAPA KUJUA


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)imeendelea  kung’ang’ania zoezi la kura ya Maoni ya kupitisha Katiba iliyopendekezwa na Bunge maalum la Katiba ifanyike tarehe 30 April mwaka huu,Anaandika KAROLI VINSENT.Endelea nayo.
     Kwa mujibu wa Tamko lilitolewa leo Jijini Dar es Salaam na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kusainiwa na Kaimu mkurugenzi wa (NEC) Dk. Sist Cariah linasema zoezi la upigaji wa kura ya maoni lipo pale pale ambayo ni tarehe 30 April mwaka huu.
     Na kwamba taarifa zilizoripotiwa na Vyombo vya Habari pamoja na mitandao ya kijamii zikimnukuu Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya uchaguzi nchini (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva  kwamba tume hiyo itaongeza mda wa kura ya maoni kutokana na kushindwa kuwaandikisha watu nchi nzima kwa mwenzi mmoja uliobakia sio za kweli.
       Akifafanua taarifa hizo Dk Cariah anasema kwamba taarifa hizo hazina ukweli na kwamba tume bado inahakika itamaliza zoezi la kuwaandisha wananchi kwenye Daftari la kupiga kura kwa mda uliopangwa na kura ya maoni kufanyika tarehe ile ile ya 30 April mwaka huu.
       Amebainisha kuwa kama wataitaji kuongeza mda watawaambia wananchi ila kwa sasa,Tume hiyo imeona hakuna ulazima wa kufanya hivyo kutokana na kuwepo mda wa kutosha kuwaandikisha wananchi kwenye Daftari la kupiga kura kwa mfumo mpya wa Biometric Voters Regislation,(BVR).
       Kauli ya Tume hiyo uchaguzi inakuja ikiwa ni siku chache kupita baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuutangazi ulimwengu kuwa kura ya maoni itafanyika tarehe 30 April mwaka huu.
     Kauli hizo za (NEC) pamoja na Waziri mkuu Mizengo Pinda zimekuwa zikipingwa na wanasiasa pamoja wanaharakati wakisema kura ya maoni haiwezi kufanyika kwa mda waliopanga kutokana na tume hiyo ambayo sasa ipo katika mkoa wa Njombe ambapo wametumia zaidi ya mwezi mmoja sasa kwahiyo kwa mwezi mmoja uliobaki hawawezi kukamilisha kuwaandikisha  watu wa mikoa zaidi ya 22 kwa mwezi mmoja.
    Kwa Mujibu wa Mtoa Taarifa wetu kutoka Kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC ameumbia Mtandao huu kwa sasa kinachosema na viongozi wa tume hiyo pamoja na viongozi wa Serikali kulazimisha kura ya maoni kufayika kwa mda huo ni kujidanganya.
       “Sikufichi hapa tunafosiwa na Rais tufanye tuwezavyo tuwe tumemaliza Mwezi wa nne wakati uwezekano ni mdogo,kwasababu Daftari la kudumu haliwezi kukamilika kwa mda huo.yaani kama vifaa vikiwepo vyote vinavyoitajika basi  Daftari  linaweza kukamilika mwishoni mwa mwezi juni,yaani hapa hata wafanyaje  hiyo kura haipigiki mwezi wanne”ameeleza.
      Taarifa za Kumanika ambazo mtandao huu umedokezwa zinazidi sema hadi kufikia jana,NEC ilikuwa na mashine 250 tu za kuendesha zoezi hilo,huku matatizo mengi yakiwa yamejitokeza katika uandikishaji wake unaoendelea Mji mdogo wa Makambako Mkoani Njombe.
       Licha ya vifaa hivyo kuwa vichache tayari nchi jirani ikiwemo Kenya wameigomea Serikali nchini ambayo ilikuwa inataka kuazimwa mashine hizo za (BVR)
        Mtoa taarifa huyo alizidi kuambia mtandao huu kwamba Shehena ya Mwisho ya Vifaa inatarajiwa kuwasili nchini katikaki ya  mwezi Juni mwaka huu.
       Kwa mujibu la Andishi laNEC lilisema tume hiyo inahitaji mashine 15,000,Lakini serikali imeridhia kununuliwa mashine 8000,jambo la kushangaza NEC imepewa Mashine 250 tu kuendesha zoezi hilo ,Mradi huo ambao unagharimu zaidi ya Bilioni 293 za kitanzania.
           Kulazimishwa huko na Rais Kikwete kwa tume ya uchaguzi  ili kuharakisha uandikishaji wa wapiga kura kunakuja huku ikiwa tayari vyama vikuu vya Upinzani nchini kupitia umoja wao,kutaka kura hiyo ya Maoni isitishwe  kwa kuwa haitoweza kufanyika kwa ufanisi na kwamba badala yake serikali iwekeze nguvu zake katika kufanikisha uchaguzi mkuu utakofanyika baadae mwa mwaka huu.
         Mbali na Vifaa vya uandikishaji huo,kumekuwa na mapungufu mengi yamejitokeza ambao watendaji wa NEC wamethibitisha kutokea.
        “Waandikishaji wanababaika,watu wengi,wanapanga foleni kutwa zima,halafu mara waambiwa kamera,halafu mara wanaambiwa mashine mbovu tena wanaambiwa kamera imegoma”

   “La ajabu zaidi tumeshuhudia mashine imeshindwa kusoma alama za vidole wenye usugu” ameeleza mtoa taarifa wetu wa NEC aliyoko Makambako

No comments