KIMENUKA TENA-MCHUNGAJI MTIKILA AZUIA MAHAKAMA YA KADHI MAHAKAMANI,SOMA HAPA KUJUA
MCHUNGAJI Christopher
Mtikila, leo amefungua kesi ya kikatiba namba 14 ya mwaka 2015 katika Mahakama
Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa mabadiliko ya sheria kwa ajili ya kuitambua
rasmi Mahakama ya Kadhi. Deusdedit Kahangwa anaripoti…(endelea).
Muswada huo umepangwa
kuwasilishwa, kujadiliwa na kupitishwa katika kikao cha Bunge litakaloanza
vikao vyake Jumanne wiki hii mjini Dodoma.
Katika mashtaka yake,
Mchungaji Mtikila aliye Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Democratic (DP),
anaitaka mahakama kuu kufanya mambo makuu matatu.
Kwanza, anaitaka imwadhibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, George Masaju, kwa kumpa kifungo kisichopungua miaka mitano kutokana
na kitendo chake cha jaribio la kuvunja ibara ya 19 ya Katiba ya Tanzania ya
mwaka 1977.
Pili, anaitaka itamke kwamba ni kinyume
cha sheria kwa serikali kujihusisha katika masuala yoyote yanayohusu Mahakama
ya Kadhi au Shirika la Waislamu Duniani (OIC).
Na tatu,
anaitaka Mahakama Kuu itamke kwamba adhabu zinazotolewa na Mahakama ya
Kadhi kwa mujibu wa sheria za Kiislam (sharia), kama vile viboko, kupondwa mawe
hadi kufa, kukata kichwa, na kukata mikono, zinapingana na utu wa binadamu, na
ni kinyume cha Tamko la Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka
iliyo mikononi mwa MwanaHALISIOnline, mshitakiwa mkuu ni Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, George Masaju, ambaye ni mshauri mkuu wa serikali kuhusu masuala yote
ya kisheria. Masaju anakabiliwa na mashtaka makuu mawili.
Kwanza, Mtikila
anamtuhumu Masaju kushirikiana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mawaziri Mary
Nagu, Asha-Rose Migiro na mawakala mbalimbali katika kuratibu uanzishwaji wa
“Mahakama ya Kadhi” kazi ambayo ni sehemu ya mradi mpana wa “kuibadilisha
Tanzania kuwa dola ya Kiislam.”
Kwa mujibu wa Mtikila hili ni
jaribio la “kuipindua serikali ya kidemokrasia na isiyofungamana na dini yoyote
katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” na badala yake kusimika mfumo wa
serikali yenye mnasaba na dini ya Kiislam “chini ya usimamizi wa makadhi.”
Mtikila anadai kwamba,
kwa mujibu wa sheria za Kiislam (sharia), kiongozi aitwaye “Kadhi Mkuu”
anapaswa kuwa na mamlaka ya pili baada ya rais wa nchi.
Hivyo, anasisitiza
kuwa mfumo huu wa kisheria utawainua waislamu wapatao milioni 12.4 dhidi ya
Wakristo wapatao milioni 29 hapa nchini Tanzania.
“Muswada kuhusu Mahakama ya Kadhi
haukubaliki Tanzania kwa kuwa ni wa kibaguzi, kwani unawahusu Wasislam pekee
ambao ni sehemu ndogo ya wananchi, na hivyo utawafanya wananchi baki kuwa
watumwa wa waislam, jambo ambalo ni kinyume cha ibara za 12, 13(2), 13(4),
13(5) na 19 katika Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977,” anasema Mtikila.
Kwa mujibu wa Mtikila
Wakristo hao milioni 29 wanajumuisha Walutheri milioni 5.5, Wakatoliki milioni
11, Waanglikana milioni 3, Wamoraviani milioni 1.8, Wapentekoste milioni 5.8,
Waadventisti milioni 1.8 na waumini wa dini za asili milioni 7.
Pili, Mtikila anamtuhumu Masaju
kushirikiana na Waziri Stephen Wasira, Mizengo Pinda, Ernest Ndikilo, Karen
Yunus, Issa Njiku, Dan Makanga, na Ernest Mangu kusigina katiba ya nchi kwa
kuwaweka Wakristo milioni 29 chini ya utumwa wa Kiislam, kwa kuwazuia kuchinja
mifugo yao kwa ajili ya kitoweo, na badala yake kuwataka wale kitoweo kutokana
na wanyama waliochinjwa na Waislam.
Kwa mujibu wa
mchungaji Mtikila, jambo hili ni kinyume cha Sheria ya Magonjwa ya Wanyama ya
mwaka 2003; kinyume cha Sheria ya Chakula, Madawa na Vipodozi ya mwaka 2003; na
kinyume cha ibara ya 19 ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.
Kwa kuzingatia tuhuma hizi,
Mtikila anaiomba Mahakama Kuu kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na
washirika wake kujieleza ni kwa nini wasifungwe jela kwa miaka mitano na zaidi
kwa kosa la kuisigina katiba ya nchi ambayo walikula kiapo cha kulinda na
kuitetea.
Mtikila amefungua
mashtaka hayo kwa kutumia mamlaka yake kama raia wa Tanzania mwenye jukumu la
kuilinda katiba ya nchi dhidi ya dharau na usiginaji mwingine wa aina yoyote.
Mamlaka hayo anapewa na ibara ya 26(2) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.
Chanzo ni
Mwanahalisi.oline
Maoni 3
Naunga mkono hoja ya mtikila amefafanua kilichopo so anatoa kitu cha msingi make mahakama ya kadhi imekua ikitumika kisiasa zaidi
Mtikila amekuwa smart kwa kumulika Watanzania waone na kubaini full package inayoenda pamoja na mahakma a Kadhi.
Mikataba mingi inayolitesa Taifa hili isingesainiwa kama wenye dhamana ya uongozi wangeangalia full package ya masharti yake.
Nasi tunajua kuwa kitu pekee kinachoweza kumpofusha asiye kipofu, akasaini kama vile haoni, RUSHWA.
Hata mtu akipewa cheo asichostahili, hiyo nayo ni rushwa ya kumsukuma afanye maamuzi bila kutumia akili zake, bali kumfurahisha aliyemtea.
Kwa hiyo ipo haja pia watu wachunguzwe kama wana sifa za kutosha kushika nyadhifa walizonazo.
Hapo sawa. Mtikila umepevuka!!
Chapisha Maoni