Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO.NI VITA MAASKOFU NA MASHEHE,WAISLAM WATOA MASHARTI MAZITO KWA KIKWETE,WAIRUSHIA KOMBORA BWAKWATA,SOMA HAPA KUJUA

Pich ani niNaibu Katibu Mkuu Taasisi ya Kiislam nchini
 Sheikh Rajab Katimba
Akuzungumza na wanahabali leo

NA KAROLI VINSENT
TAASISI ya dini ya Kiislam imeita serikali kuwakamata maaskofu na wachungaji ambao wanadai wametoa matamko ya kichochezi na endapo serikali ikikaidi kuwakamata, basi jumuiya hiyo itawahamaisha waamini wa dini ya kiislam popote walipo kuipigia kura ya Hapana Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
     Kauli ya taasisi hiyo yenye misimamo mikali inatokana na Tamko walilotoa muunganiko wa jumuiya ya Kikristo,ikiwemo Baraza la Maaskofu katoliki (TEC),Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT),Baraza la Makanisa la kipentekoste(CPCT)ambao wote  kwa pamoja waliiwataka waunini wa dini ya kikristo nchini kuipigia kura ya hapana katiba,kutokana na serikali  kuruhusu mahakama ya Kadhi kisheria.
      Akitoa tamko la Taasisi ya Dini ya Kiislam  ambalo ni muunganiko wa taasisi ya dini hiyo zaidi ya 11 hapa nchini ,Naibu Katibu Mkuu Taasisi hiyo Sheikh Rajab Katimba wakati wa Mkutano na Vyombo mbalimbali vya Habari leo Jijini Dar es Salaam-
        Ambapo Sheikh Katimba huku akiongea kwa uchungu ameitaka serikali iwachukulie hatua maaskofu hao kwa madai ya kufanya uchuchezi na kuvunja katiba ya nchi.
      “Serikali iwachukulie hatua za kisheri maaskofu na wachungaji kwa kutoa matamko yakichochezi yaliyokusudia kuumiza hisia ya kidini kwa waislam kinyume cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 ikiwemo kuwakamata,kuwafikisha mahakamani na kuzuia dhamana kama inavyofanya kwa masheikh pindi wanapotoa kauli zinazopingana na mtazamo wa serikali lasivyo hatutaipigia kura katika iliyopendekezwa”amesema Seikh Katimba.
      Sheikh Katimba ameongeza kuwa Serikali imetoa rushwa kwa Waislam na kwa kundi maalum kwa kukubali sheria itakayounda mahakama ya Kadhi ili kuipitisha katiba iliyopendekezwa ambapo amesema ni kuidhalilisha dini ya mwenyezi mungu ikiwemo kuwadhalilisha waislam na ni kuumiza hisia ya waislam na kuhatarisha amani na utangamano.
       Amebainisha kuwa Serikali iendelee na Mchakato wa uundwaji mahakama ya kadhi kwa kufuata maoni yaliyotolewa mbele ya kamati ya sheria na utawala wa bunge kwa kuzingatia mambo muhimu.
      Aliyataja mambo muhimu hayo ikiwemo ni serikali iache njama anazodai na hila za kuigeuza mahakama ya Kadhi inayohitajika kuwa miliki ya taasisi ya BAKWATA na MUFTI wa BAKWATA.
        “Endapo serikali itaendelea na kuwasilisha muswaada wa Mahakama ya Kadhi unaoipa mamlaka Bakwata kuunda,kusimamia,kuteua makadhi nakadhalika kinyume na maoni ya Waislam wengi itakuwa imethibitisha kuwa serikali haikuwa na nia ya kweli ya kuunda na kuanzisha mahakama ya Kadhi”ameendelea kusema Sheikh Katimba
     Aidha,Sheikh katimba amesema serikali igharamie mahakama hiyo kama ambavyo anadai serikali hivi sasa inavyogharimia uendeshaji wa mashauri yaliyopo kwenye mahakama za kawaida yanayohusu sheria za kiislam ambayo mara nyingi yanaamuliwa kwa makosa.
“Na pia igharamiwe na serikali ambavyo serikali hii inavyogaramia huduma za makanisa chini ya mkataba maarufu memoradum of understanding (MOU)mkataba  ambao haukuwahusisha wala kutaka ridhaa ya waislam”ameongeza kusema



No comments