EXCLUSIVE-WAUAJI WA DOKTA SLAA HAWA HAPA,VIGOGO WA USALAMA WA TAIFA WATAJWA SOMA HAPA KUJUA
ELISIFA Ngowi, naibu mkuu wa usalama wa taifa mkoa wa Dar es
Salaam, ni miongoni mwa waliopanga mkakati wa kuangamiza maisha ya Dk.
Willibrod Slaa. Anaripoti Deusdedit
Kahangwa…(endelea).
Ngowi ni mmoja wa watu 30 wanaotajwa
kupanga njama za kumuua Dk. Willibrod Slaa kwa “…sumu au njia nyingine ambazo
zisingegundulika.”
Kwa
mujibu wa mawasiliano katika simu ya Khalid Kangezi, mmoja wa walinzi wakuu wa
Dk. Slaa, aliyekiri kushiriki njama za kumuua mwanasiasa huyo shupavu,
yanaonyesha orodha ndefu wakiwamo waliotajwa kuwa maofisa wa idara ya usalama
wa taifa (TISS).
Ngowi ni mmoja wa watuhumiwa muhimu
katika wizi wa fedha za umma katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). Alikwapua
mabilioni ya shilingi kupitia kampuni yake ya Clayton Marketing Ltd na
Excellent Services Ltd.
Kampuni ya Ngowi – Clayton
Marketing Limited – ni miongoni mwa kampuni 22 yaliyochotewa na serikali kiasi
Sh. 133 bilioni kutoka BoT.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa
na Kangezi na baadaye kuwasilishwa kwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kinondoni,
Camillius Wambura, Ngowi ni miongoni mwa waliopanga mkakati wa kumuua Dk. Slaa,
ulitakiwa kutekelezwa kabla ya mwisho wa Aprili mwaka huu.
Mwingine anayetajwa kupanga njama za
mauaji hayo, ni Philiph Mangula, makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Tanzania Bara.
Kagenzi anasema, “Mpango wa
kumdhuru Dk. Slaa niliuanza tangu tarehe 8 Julai 2014, tukiwa Kituo cha
Demokrasia (TCD), Ilala Dar es Salaam. Mawasiliano haya nilianza kufanya
kupitia kwa Burton Mn’gen’ge, ambaye ni msaidizi wa Mangula.”
Anasema, “Huyu bwana alinishawishi
kuwa nampa taarifa za siri za chama, pamoja na Dk. Slaa binafsi. Watu hawa
wamekuwa wakinipa fedha za muda wa maongezi ili kufanya mawasiliano nao na
fedha nyingine kwa ajili ya matumizi mengine.”
Kangezi anataja namba mbili za simu
yake ambazo zimekuwa zikifanya mawasiliano mfululizo na washirika wake kuwa ni
0764 367750 iliyosajiliwa kwa jina la Sudi Juma na 0763 848530 iliyosajiliwa
kwa jina la Khalid Kangezi.
Namba nyingine ya Kangezi ni Na.
0652 215875 ambayo alitumia kwa mawasiliano yake na Ngowi na “washirika wake.”
Ngowi katika mawasiliano yake na
Kangezi, alitumia simu zake mbili ambazo ni Na. 0713 340770 na 0754 340770.
Katika maelezo yake yaliyorekodiwa
mbele ya Kamishna wa kiapo, John Malya, Kangezi anasema, amekuwa na mawaliano
na maofisa usalama na viongozi ngazi ya juu katika CCM.
Njama za kutaka kumdhuru na, au
kumuua Dk. Slaa zilivujishwa hadharani kwa mara ya kwanza na Mabere Marando,
wakili wa mahakama kuu na mwanasheria wa chama hicho.
Alisema, chama chake
kimejiridhisha kuwa mawasiliano kati ya CCM na usalama wa taifa, yamekuwa
yakilenga kutoa maisha ya Dk. Slaa.
Taarifa zinasema, waliompa kazi
Kangezi, walitaka kuwasilisha kwao, taarifa ya kila ambacho Dk. Slaa anatenda,
ikiwamo taaarifa ya majadiliano ya vikao vya chama, pamoja na kutaja majina ya
watu wanaokutana naye.
“Tarehe 28 Februari 2015,
nilikuwa na Gwamaka Mwan’gonda pale Magomeni hospitali, karibu na ofisi ya mkuu
wa wilaya.
Nilikutana naye hapo akiwa na gari T 213
ARS. Tuliondoka na mazungumzo yaliyokuwa ndani ya gari, ni kunishawishi
kukubali kumuua Dk. Slaa,” anaeleza Kangezi.
Naye Mangula alikuwa akifanya
mawasiliano na Kangezi, kupitia simu yenye Na. 0764 532222.
Kangezi anasema alikabidhiwa chupa
ndogo ya kioo inayolingana na kichupa cha plastiki, ambayo aliihifadhi nyumbani
kwake ili kutekeleza mauaji hayo.
Wengine ambao Kangezi amekuwa
na mawasiliano mfululizo, ikiwamo kutumiwa fedha kwa njia ya simu, na ambao
walikuwamo katika njama za mauaji hayo, ni Lilian Mduma na Edward Lyombe.
Lilian Mduma na Lyombe, ni wasaidizi
muhimu wa Mangula. Lyombe anatumia simu tatu ambazo ni 0757 067390, 0786 873020
na 0714 280 111.
Naye Lilian, katika
mawasiliano yake na Kangezi anatumia simu Na 0719 795222.
Wengine waliomo katika mpango
huo, Gwamaka, Fahami Alnahdi, Dominic Gama na Vicent Shayo.
Fahani katika mkakati wake huu
na Kangezi alikuwa anatumia simu Na. 0713 522222; Gama alikuwa akitumia simu
mbili ambazo ni 0754 000666 na 0786 220066 na Mn’gen’ge akitumia simu tatu
zenye Na. 0712 386 505, 0769 916331 na 0778 558888.
Katika maelezo yake yaliyopelekwa
polisi na maofisa usalama wa Chadema, Kangezi anasema, “Mzee Philiph Mangula, nimekuwa nikiwasiliana
naye kupitia simu yake Na. 0764 532222 kwa kunipigia mara kadhaa.”
Anasema, “…mzee Mangula
amenitumia vocha (muda wa maongezi) mara mbili kiasi cha Sh. 50,000 (elfu
hamsini). Lakini Alhamisi ya 4 Desemba mwaka jana, ndipo aliponitumia kiasi cha
Sh. 150,000 (laki moja na elfu hamsini) ili nimpatie taarifa za siri za chama
na kumpigia simu nikiwa katika vikao mbalimbali.”
Siku ambayo Kangezi alipokea
fedha kutoka kwa Mangula, Dk. Slaa alikuwa akihudhuria kikao cha kamati kuu ya
chama chake.
Kangezi anakiri pia kuwa amewahi
kutoa taarifa kwa “waajiri
wake” hao kuhusu nyendo za Dk. Slaa, ikiwamo katika mikutano yake na mabalozi
na watu wengine mbalimbali.
Anasema, amefanya mawasiliano na
Lyombe kumjulisha kuwapo kwa mkutano kati ya Dk. Slaa na mabalozi wa Jumuiya ya
Ulaya (EU), jijini Dar es Salaam.
Mawasiliano hayo aliyafanya
saa 5:16 asubuhi. Dk. Slaa aliingia katika mkutano huo, majira ya saa tano kamili.
Chanzo ni
Mwanahalisi.oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni