SASA NHIF YAPELEKA MADAKTARI BINGWA MIKOANI, NIA NI KUWAFANYA WAKAZI WA MIKOANI NAO KUNUFAIKA NA MATIBABU.
SELEMANI MAGALLI.
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeendelea na jitihadazake za kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya afya iliyo bora kwa kuamua kupeleka madaktari bingwa katika mikoa ya pembezoni kwa ajili ya kutoa huduma za kitaalam kwa wakazi wa maeneo hayo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuona kuna haja ya madaktari bingwa kufika katika maeneo ya mikoani kufuatia tathimini ambayo imefanywa katika mikoa ya Lindi na Kigoma ambako kulionekana kuwa na haja ya wataalam kwenda huko haraka ili kutibu watu
Kupeleka kwa madaktari hao kunatokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali zikiwemo
za uchache wa madaktari hao,umbali wa hospitali kubwa zenye huduma hiyo au
changamoto za Kijiografia zinazozuia kufika kirahisi pamoja na za
kimiundombinu.
Akizungumza na mtandao huu mapema hii leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kitabibu na Kitaalam wa NHIF,Dkt. Aifena Mramba amesemaNHIF imefikia uwamuzi huo ili kufanya wakazi wa mikoa iliyopembezoni mwa Dareslaam nao kufaidika na mfuko huo wa Taifa
Akizungumza na mtandao huu mapema hii leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kitabibu na Kitaalam wa NHIF,Dkt. Aifena Mramba amesemaNHIF imefikia uwamuzi huo ili kufanya wakazi wa mikoa iliyopembezoni mwa Dareslaam nao kufaidika na mfuko huo wa Taifa
Aidha DK Mramba ameendelea kusema kuwa kwa sasa kuna jumla ya madaktari bingwa 4 ambao wote hawa watapitia katika hospitari za mikoa iliyochaguliwa kwa mtindo wa mzunguko na kwamba amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kwenda kuangaliwa na madaktari Bingwa
Dk Mramba amesemahiyo ni awamu ya tatu na kwamba mikoa ambayo
ilipata huduma za matibabu kutoka kwa madaktari bingwa katika awamu ya kwanza
ni mikoa ya Lindi na Kigoma,ambapo awamu ya pili ilikuwa ni mikoa ya
Rukwa,Katavi na Pwani.
Awamu ya tatu ya mpango
huo inahusisha mikoa ya
Mara,Tabora,Manyara na Mtwara,ambapo waliopata huduma hiyo ni 5,829 kati ya hao
153 walifanyiwa upasuaji.
Dkt. Aifena amesema kupeleka huduma ya madaktari bingwa ni kutokana na mafanikio yaliyotokana na NHIF kubaini kuwa kuwa Watanzania wengi wanahitaji huduma za madaktari bingwa na madhumuni ya mpango huo ni kushiriki katika kufanikisha lengo la serikali la utoaji wa huduma bora za afya kwa watu wote na kuleta wa unafuu kwa wananchi wa pembezoni au mikoa iliyo mbali na huduma za hizo.
NHIF inagharamia uwepo wa
madaktari hao,vifaa tiba na dawa zinazotumika katika zoezi hilo na
mwitikio wa wananchi ni mkubwa ikilinganishwa na madaktari bingwa
pamoja na changamoto za vifaa tiba vya kisasa katika baadhi ya
hospitali,uhaba wa vitendanishi vya kupimia,miundombinu na uhaba wafanyakazi
wenye uzoefu ili kusaidiana na madaktari bingwa
Hakuna maoni
Chapisha Maoni