Zinazobamba

NHIF WAKUTANA NA VYAMA VYA SACCOSS TEMEKE, WAWAPIGA MSASA KUHUSU UMUHIMU WA KUJIUNGA NA MFUKO HUO KWA WATU WASIO KATIKA SEKTA RASMI


Meneja  wa Bima ya Afya NHIF  Wilaya  ya  Temeke, Bi Ellentruder Mbogoro (anayehojiwa), akizungumza na waandshi wa habari kuhusu mafunzo ya siku moja kwa viongozi wa Saccos yaliolenga kutoa elimu juu ya umuhimu wa wanachama wa Saccos kujiunga na mfuko wa bima ya Taifa. Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Bw. Rehani Athumani mapema hii 
2
Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Bw. Rehani Athumani akifungua mafunzo ya siku moja ya viongozi wa SACCOS Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam lengo la mafunzo hayo ni kuwapa elimu kuhusiana mpango wa kujiunga na NHIF kupitia vikundi (KIKOA) ili wapate uhakika wa matibabu kupitia mfuko wa bima ya afya. 


Afisa matekelezo na uratibu (HQ) ambaye pia ni  kaimu meneja wa mfuko wa afya kwa jamii  Bw. Salvatory Okumu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo hayo kwa viongozi wa vikundi vya saccos katika wilaya ya Temeke. Okumu amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo viongozi wa Sacoss ili nao wawaeleze wanachama wao umuhimu wa kujiunga na mfuko wa bima ya afya kupitia mpango huu mpya wa KIKOA.

Afisa ushirika mwandamizi wa wilaya ya TemekeBi.Zaina Musa Mahomba akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo kwa  viongozi wa Saccoss,Mahomba amesema mfumo huo mpya ambayo shirika hilo la bima ya Afya limekuja nalo utawasaidia sana wananchi hususani hawa wanachama katika saccoss. Jumla ya washiriki 100 wameshiriki katika mafunzo hayo.

Baraka Mwakamola ambaye ni afisa ushirika wilaya hiyo ya Temeke akifafanua jambo kwa waandishi wa habari. Mwakamola amewataka wanachama wa saccoss kukimbilia fursa hiyo haraka kwani inakupa unafuu wa kupata matibabu kwa haraka na uhakika. Ili mwanachama ajiunge anahitajika kuchangia kiasi kidogo ambacho siyo chini ya shilingi elfu 70 kwa mwaka.

Viongozi  wa vyama vya Saccos wilaya ya Temeke wakifuatilia mafunzo hayo ya siku moja kutoka kwa mwezeshaji. Wanachama watakaojiunga na huduma ya NHIF watanuafaika na kupata matibabu bure kwa kipindi chote cha mwaka mzima.


Mfuko wa bima ya Afya wilaya ya temeke imeendesha warsha ya sikumoja kwa viongozi wa Saccos katika wilaya hiyo yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya SACCOS kuhusu  mpango wa NHIF wa KIKOA unaotolewa na Bima ya Afya ili waweze kujiunga na Mfuko huo 

Akizungumza na Mtandao huu mapema hii leo,Meneja  wa Bima ya Afya NHIF  Wilaya  ya  Temeke, Bi Ellentruder Mbogoro amesema wamefikia hatua hiyo ya kuwajengea uwezo viongozi hao ili waweze kufahamu mpango wa Kkoa madhumuni yake hasa na hivyo kuwashawishi wanachama wao waweze kujiunga na mfuko ili wanufaike na uhakika wa matibabu kupitia mfuko wa bima ya afy.

Aidha katika hatua nyingine viongozi wa Saccos ambazo zimehudhuria katika mafunzo hayo wamekili kuona umuhimu wa kujiunga na Mfuko huo wa bima ya afa na kwamba wameahidi kupeleka elimu hiyo kwa wanachama wao ili nao wapime na baadae waamue kujiunga na mfuko kwani inaumuhimu mkubwa mno
Akizungumza na mtandao huu, Kasali Mgawe ambaye ndiyo katibu wa Saccos ya vijana wialaya ya Temeke, amesema Mafunzo hayo ni muhimu na yamewafungua macho, kwani gharama ya 70000 kwa mwaka si nyingi ukiangalia na gharama halisi kama utaumwa hapo katikati.

Hakuna maoni