Zinazobamba

HIVI NDIVYO CHADEMA WALIVYOJIPANGA KWA UCHAGUZI, WAVAMIA VYUO MBALIMBALI WAANZA NA CHASO- NIT


Mgeni rasmi katika siku ya kuzindua tawi la CHASO NIT Mwanasheria Tundu Lissu akiingia katika viwanja vya Nit tayari kufungua Tawi jipya la wanachadema chuoni hapo, Jumla ya vijana 200 walifanikiwa kupata kadi ya chama cha chadema kutoka kwa mwanasheria huyo.

Mbunge wa Jimbo la ubungo ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa chama cha chadema akiingia katika viwanja hivyo vya nit tayari kwa uzinduzi wa CHASO- NIT mapema hivi karibuni. Katika uzinduzi huo, mbunge huyo aliwataka viongozi wa chini yake kuhakikisha wanaanza kufikisha moto huo katika vyuo vingine ili wanafunzi waanze kuendesha vuguvugu la mabadiliko na hivyo kukomboa taifa kutoka kwa mafisadi wachache.




Tundulisu na mbunge wa jimbo la Ubungo BW. John John Mnyika wakipitia makabrasha yao kabla ya kuanza kikao cha kuzindua tawi la wanafunzi wanaopenda chama cha chadema katika chuo cha taifa cha usafirishaji huko mabibo jijini Dareslaam, wanafunzi kibao walichukua kadi

Mwenyekiti wa Chaso-NIT Bw. Danyy Nyamuhanga akitambulisha makamanda wake waliojitoa kuhakiksiha kazi ya kuanzisha tawi la vuguvugu la kukomboa watanzania kupitia chadema,

mwenyekiti Nyamuhanga akitoa maelekezo kwa mwanasheria mkuu wa chama cha chadema ambaye pia ni mbunge na waziri kivuri wa sheria na katiba siku ya kufungua tawi la Chaso -NIT mapema hivi karibuni. Mbunge huyo alikuwa akijitayarisha kutoa kadi kwa wanafunzi wa Nit.

Makamanda wapya toka chuo cha taifa cha usafirishaji wakipokea kadi kutoka kwa TUNDULISU mapema hivi karibuni. Tundulisu aligawa kadi zaidi ya 200

Tundulisu akizindua tawi hilo la CHASO NIT kwa kufunga Bendera ya chama katika tawi hilo jipya kwa chuo cha taifa cha usafirishaji.

Hakuna maoni