HABARI NJEMA-PATO LA TAIFA LAKUA KWA KASI,TAKWIMU YASEMA HALI NI NJEMA SOMA HAPA KUJUA
Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Picha na Maktaba |
PATO la Taifa limeongezeka kwa kasi ya asilimia 6.8 katika kipindi cha robo ya tatu mwaka 2014 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 7.4 katika kipindi kama hicho cha mwaka 2013.Anaripoti KAROLI VINSENT,Endelea nayo.
Hayo yametangazwa mda huu jijini
Dar es Salaam na Mkurugenzi uchumi na Fedha wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bwana
Morrice Oyuke Wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari ambapo amesema Matokeo
ya Takwimu za pato la Taifa kwa robo mwaka kwa bei ya miaka inayohusika
yameonyesha -
kuwa thamani la pato la taifa katika
kipindi cha robo tatu ya mwaka 2014 ilikuwa trilioni 21.2 kwa mwaka 2014
ukulinganishwa na 19.8 trilioni kwa mwaka 2013.
Bwana Oyuke ameongeza kuwa pato la
taifa kwa bei za mwaka 2007 katika kipindi cha robo mwaka ya tatu linaonyesha
kuwa jumla ya thamani ya 10.7 trilioni
mwaka 2014 ikilinganishwa na 10.1 trilion kwa mwaka 2013 katika kipindi
hicho.
Alibainishwa kuwa ukuaji wa pato
hilo umetokana na shughuli za kiuchumi ikiwemo-
Ukuaji wa Sekta ya Kilimo na Mifugo
ambapo zilikuwa kwa asilimia 3.1 katika kipindi cha robo mwaka ya tatu ya mwaka
2014 ukulinganisha na kasi ya ukuaji wa asilimia 3.4 kwa mwaka 2013.
Mbali na hizo alizitaja shughuli zengine ni za uchumi za viwanda na
ujenzi ,shughuli za uchimbaji wa madini,mawe,shughuli za uzalishaji nisharti ya
umme,uzalishaji wa viwandani ambazo zote kwa pamoja zimekuwa kwa kasi kubwa
ukilinganisha na mwaka 2013
Hakuna maoni
Chapisha Maoni