HABARI KUBWA LEO-DILI LA KATIBA MPYA LAVUJA,NI LA RUGE WA CLAUDS RADIO NA MAKONDA SOMA HAPA KUJUA
RAIS KIKWETE |
IKULU ya
Rais Jakaya Kikwete bado inaendelea
kulazimisha katiba iliyopendekezwa na
Bunge maalum la Katiba kupigiwa kura ya ndio na wananchi ,huku ikiwa kinyume
na sheria ya kura za maoni.Anaripoti KAROLI VINSENT endelea nayo .
Habari za kuaminika ambazo mtandao huu
umezipata zinasema kwa sasa kumekuwa na mpango unaoandaliwa na Ruge Mutahaba na
kusukwa kwa karibu paul Makonda,Katibu wa uhamisishaji wa Umoja wa vijana wa
Chama cha Mapinduzi CCM,mpango huo wenye kugharimu Sh.Milioni 588.4 za
kitanzania.
Mpango huo unaratibiwa na
kinachoitwa “Kamati ya kusimamia
utangazaji wa katiba iliyopendekezwa”
iko chini yaOfisi ya Ikulu.
Ruge ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni
ya Clouds media ambayo inamiliki Radio ya Clouds Fm,Clouds Tv ambapo
amependekeza fedha hizo zitumike kwa ajili ya kugharamia vyombo vya Habari,wasanii
wa kizazi kipya,mchiriku na muziki wa Taarabu.
Kwa mujibu wa sheria ya kura ya
maoni unaiumbua Ikulu ya Rais Kikwete baada ya sheria hiyo kusomeka kwamba kura
ya maoni ,Serikali haipaswi kuegemea
upande wowote katika pande mbili –inayounga mkono katiba inayopendekezwa au
inayopingwa.
Kuibuka kwa mipango hiyo ambayo
serikali imekuwa na mradi wake huu,kumekuja takribani miezi miwili baada ya
kuvuja mkakati wa kwanza uliokuwa unaratibiwa na ikulu na ulikuwa unatafuta
kura ya "ndio" kwa Katiba iliyopendekezwa.
Mkakati huo uliibuliwa na Katibu mkuu
wa Chama cha Maendelea Chadema Dk Wilbroad Slaa ambapo Slaa aliwaambia
waandishi Habari kuwa Mkakati huo aliunasa ulikuwa unatoka kwa Katibu Mkuu wa
Rais kwenda kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Salva Rweimamu.
Katika Andishi hilo Mkurugenzi huyo wa
mawasiliano ya Rais alishauri bajeti ya Sh.Bilioni 2.5 .mkakati huo ulikuwa
unapangwa kuwalaghai wananchi kuipigia kura ya Ndio katiba iliyopendekezwa na
bunge Maalum la Katiba.
Waraka huo ambao Salva,alikiri kuwaandaa
na kusema kikao cha awali kilikuwa kinafanyika na kuwashirikisha wahariri wa
Vyombo vya Habari nchi.
Ambao ni Assah Mwambene Mkurugenzi wa
Maelezo,Saidi Yakubu afisa mwandamizi kutoka ofisi ya Bunge,Gabriel Nderumaki
Mhariri Mtendaji wa Magazeti Ya Serikali,Joseph Kulagwa mhariri mtendaji wa
Gazeti la Chama cha Mapinduzi CCM la Uhuru na Mzalendo na Angel Akilimali naye
ni Mkurugenziwa Radio Uhuru.
Kwa Mujibu wa Mpango wa Ruge
Mtahaba umewataja wasanii mbalimbali
kutumika,wanaoelezwa kutumika kulaghai wananchi ili kupigia kura ya ndio ni
Khadija Kopa,mzee yuseph,Isha Mashauzi,Hussen Mohamed (Hammer q),Barnaba
Elias,EsterLinah Sanga,Mwasiti Almas,Mwasiti
Almas,Mataluma,Madee,Godzilla,Yamoto Band,Omy Dimpoz,Chege na Temba,Vanesa Mdee
na Hamis Mwijuma (mwana FA).
Hakuna maoni
Chapisha Maoni